Ukiwa katika matatizo ni vyema kufunga mdomo wako kuliko kutangazia umma !

10:09:00 Unknown 0 Comments




Ndege mmoja alikuwa akiruka angani majira ya baridi kali sana, akiwa angani barafu ikamzidia na akaganda na kuanguka chini.

Akiwa pale chini ya ardhi huku ameganda na hawezi kuruka, ng'ombe aliyekuwa akienda malishoni akapita pale na kumnyea ndege yule.

Mara ndege akaona kafunikwa na kinyesi na joto la kinyesi likaanza kuupasha mwili wake joto.Kwa kuwa alikuwa anashindwa kujitoa na anahisi joto mwilini mwake, kwa furaha akaanza kuimba kwa sauti.

Kwa mbali paka akasikia sauti nzuri ikiimba, akaamua asogee ili kuona ni nini kipo hapo na kinatoa sauti nzuri kama ile.

Kufika pale akagundua kuna ndege chini ya kinyesi cha ng'ombe, basi akamchukua na kumfanya kitoweo ndege yule.

Funzo

1. Sio kila mtu anayekupaka kinyesi (pakazia maneno mabaya) ni adui
2. Sio kila mtu anayekuokoa katika matatizo ni rafiki
3. Ukiwa katika matatizo ni vyema kufunga mdomo wako kuliko kutangazia umma !


Tafadhali kumbuka kulike facebook page yangu Bofya hapa ku-like

You Might Also Like

0 comments: