Natamani kuwa mtu maarufu nifanyeje?
Hello Fuledi,Mimi ni binti mwenye miaka 25 na nipo mwaka wa mwisho katika chuo fulani hapa Tanzania.
Nimekuwa nateseka sana kutafuta jina yaani kuwa mtu maarufu sana hapa Bongo na juhudi naona hazileti matunda.
Nimejaribu kufanya mambo mengi sana ila yanagonga mwamba,na hivi karibuni niliamua kuandika FB post kuwa natoka na msanii fulani lakini bado haijanipa umaarufu.
Naomba nifanyeje niwe maarufu, nirushie hii kwa marafiki ili wanipe njia za kukamilisha ndoto yangu ya kuwa maarufu.
Asante


0 comments: