TAFADHALI USIPITE BILA KUSOMA KAMA UNA MOYO WA HEKIMA/HURUMA NA BUSARA

21:40:00 Unknown 0 Comments


Dunia ina changamoto sana na maumivu yake pia.

Pichani ni watoto ambao wamekumbwa na njaa na magonjwa yatokanayo na kutokula chakula bora na sio kwa mapenzi yao hapana.

Chanzo ni vita zisizo na kikomo, hali ya hewa inayosababisha ukame na kutostawisha kitu.

Wengi wao familia zao zimewakimbia na wengine wamekufa na wao kujikuta wanahitaji msaada.

Hebu fikiria wewe leo una bahati gani kuwa katika sehemu isiyo na machafuko, vita, ukame njaa na kila aina ya matatizo?

Je wewe ni bora zaidi kuliko wao? Au wao wamemkosea Mungu kitu?

Fikiria ni mara ngapi unasaza chakula na kutupa bila kujali kesho itakuaje kwa sababu una hazina kubwa ya chakula eneo ulilopo?

Ndugu yangu lolote laweza kukutokea katika maisha yako na mambo yakabadilika na kuwa mabaya kuliko hawa watoto.

Mshukuru Mungu wako kwa kukupa maisha na uhai ulionao huku ukiwa unaishi kwa amani na furaha ukiwa na familia na marafiki wa kila aina wenye msaada kwako.

TAFADHALI TEMBELEA NA KU-LIKE UKURASA WETU TABASAMU NA FULEDI

You Might Also Like

0 comments: