Binti mmoja wa miaka 17 alianza biashara ya kuuza vitu nyumba hadi nyumba ili apate fedha ya chakula na ada zake na mdogo wake.
Alichukua hatua hii baada ya baba na mama kufa na kumwacha yeye na mdogo wake wakiwa njia panda kwa kukosa fedha za ada na matumizi huku ndugu wakimsaliti pia.
Aliendelea kufanya hivyo na siku moja aliamua kwenda kwa mama mmoja aliyesifika kwa roho ya huruma, pole na ukarimu wake kwa watu wenye matatizo kama ya dada huyu ili aombe ufadhili wa kumalizia muhula wake wa mwisho chuoni.
Baada ya kusimuliwa habari ile yule mama akashikwa na uchungu akalia huku akimpa hela na kumwambia, "Mwanangu, utafanikiwa maishani na utapendwa na watu na utazunguka hii dunia kama ilivyo rahisi kwa dereva mwenye gari kujiamlia safari bila ya kujali mafuta atapata wapi"
Binti yule aliondoka huku kaamini na kuufurahia ule muda alioupata na kiongea na mama hiyo.
Hivi sasa baada ya miaka mingi kupita, binti huyu ni mkurugenzi wa kampuni moja ya kusindika chakula na anatumia muda mwingi kuwa nje ya nchi zaidi kuliko nchini mwake.
Nami nakuombea uwe na ujasiri wa kuleta mafanikio katika maisha na kupendwa na Mungu.


0 comments: