Lazima machozi yakutoke

11:34:00 Unknown 0 Comments


Pichani ni mzee aishie Afghanistan ambaye alipatwa na mkasa ambao hakuutegemea na kumfanya atokwe na machozi, machozi ambayo hajui ni lini yatasita kutoka.

Jumapili moja mkewe aliondoka na baadhi ya marafiki na kwenda sokoni kwa ajili ya shopping ya chakula na baadhi ya mavazi ya familia.

Baada hya kumaliza shopping akaamua aongee kidogo na wenzake kabla ya kurudi nyumbani, muda mfupi baadae akawasili nyumbani akiwa na zawadi za familia na chakula.

Mme alijawa na hasira na kumwambia, "uliondokaje bila ya kuniachia maji ya kuoga bafuni?" mke kabla ya kuongea alipokea kibao kilichomwangusha chini.

Akiwa pale chini mme aliendelea kumpiga mpaka alipoona amechoka na kuondoka zake kwenda kutembea.

Jioni aliporudi alishangaa kuona mkewe bado yuko pale chini, na mbaya zaidi alikuwa ni marehemu tayari aliyekufa akiwa na mimba ya miezi minne tumboni.

Na baada ya kuangalia katika mfuko aliorudi nao toka shopping aliumia kuona kanunuliwa mkufu na kanzu aliyokuwa akiipenda sana.

Mzeee huyu tangu hapo hana amani nafsini mwake na amekuwa mtu wa kuomboleza na wa kulia kila akumbukapo unyama huo.

Ni mara ngapi mwanaume tumekuwa tukifanya vitendo kama hivi kwa wapenzi wetu?

Ulishawahi kujiuliza madhara yake na majuto yake baadae???

Kamwe uhusiano hauwezi kujengwa kwa mabavu au kwa mmoja kuabudiwa zaidi ya mwenzake.

Mapenzi ya dhati ni yale ya kuthaminiani, kuheshimiana na kisha wote kwa pamoja kuamini ni jukumu lenu kuwa na furaha hata kama umaskini na matatizo gani yatawaandama.

Mzee huyu kaniumiza na sikutegemea kuumia asubuhi ya leo ila kwa habari hii nadiriki kusema " R.I.P Dada yetu"

Comment R.I.P Dada yetu kisha share ili kuwafichua wanaume wenye tabia hatarishi kama ya huyu mzee wetu

Like Tabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: