Mungu anapoamua kusimama upande wetu wakati wa shida
Palitokea mzee mmoja ambaye alipata majanga kazini na hatimaye kusimamishwa kazi.Mzee huyu sio kwamba labda alihusishwa na ubadhilifu wa aina yoyote ile pale ofisini la hasha ila aliwekewa mtengo na wenzie ili aweze kunasa na hatimaye afukuzwe kazi ile na wenzake wachukue nafasi yake.
Mzee aliishi maisha ya taabu sana baada ya kuacha kazi ile kwani hata mafao yake hakupata hivyo ilimlazimu pamoja na uzee ahangaike machana kutwa ili aweze pata hela ya kuimudu familia.
Mzee alizidi kusali na kumlilia Mungu kuwa kwa nini anamuacha katika kipindi ambacho yeye anauhitaji msaada wake japo apate kitu cha kuweza kuipa familia chakula bora, malazi bora, shule bora na hata waweze kuwa na misha bora na ya kawaida kama familia nyingine za kipatocha wastani.
Baada ya kusali na kuomba kwa muda mrefu siku moja Mungu akamtokea usiku akiwa kalala na kumwambia “mwanangu umekuwa ukinililia na kuomba kwa siku nyingi, niambie ni nini unataka nikupe mwanngu”. Mzee akasema Mungu naomba unipe hata ng’ombe niweze kukamua maziwa na kuuza ili nipate kipato kama jirani yangu afanyavyo.
Kweli Mungu si athumani, Mzee yule akapata bahati ya kazi moja iliyompta hela nzuri na hatimaye akanunua ng’ombe mmoja wa kisasa ambaye alikuwa na umwezo wa kutoa maziwa lita 30 kwa siku. Pamoja na kuwa mzee yule aliuza maziwa kwa bei kubwa kidogo lakini watu walimiminika sana na maziwa yaliuzwa hata kabla mzee hatatoka zizini kwa jinsi maziwa yale yalivyopendwa na wakazi wa mji ule.
Kutokana na mauzo ya maziwa baba ilimbidi amfungulie mkewe kipenzi mgahawa wa kuuza chakula na pia samadi iliwafanya wawe na bustani nzuri ambayo kila aina ya mboga mboga na matunda vilipatikana pale. Kweli mzee yule alifurahi na kumtukuza Mungu wake na kila jumapili hakusita kutoa sadaka na hata kumshukuru Mungu wake kwa kuifanya familia kuwa na maisha bora.
Baraka zilizidi pale ng’ombe yule alipozaa na wakiwa bado wanasubiri kuanza kuuza maziwa wakapata mkataba wa kuuza maziwa yao katika kiwanda maarufu cha kuuza maziwa na mkataba huo ulikuwa ni mnono na mzee alifurahi na kuamini kuwa Mungu ameichagua familia yake katika kuipa baraka.
Mzee aliamka asubuhi alfajiri sana, akamkisi mkewe na kumkumbushwa kwamba siku hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza kwa wao kumkamua ng’ombe wao baada ya kumwachisha ndama wao kunyonya. Na kuwa siku hiyo ndio wanatakiwa kuanza kupeleka maziwa kiwandani.Basi wakashikana mikono na mkewe wakasali na hatimaye baba akatoka kwenda kuandaa maji na vitu vya kukamulia wakati mama akiamka kwenda kuwaandalia watoto chai ili wawahi shuleni.
Mzee yule alipigwa na butwaa baada ya kuona ng’ombe yule pamoja na ndama wakiwa wamekufa na wamelalachini pale bandani, mzee alilia sana na baadae ilimbidi akamwite bwana mifugoi ili awaruhusu wachinje na kuuza nyama angalau irudishe fedha.Dokta alipofika wote walishangaa kuona ng’ombe wale ndani wameoza kuwa hata nyama isingeweza kuuzwa tena.
Mzee aliomboleza kwa siku nyingi huku akimlilia Mungu na kumwambia kwanini amemwonjesha maisha mazuri na hatimaye kushindwa kumlinda mbele ya maadui zake ambao wanamrudisha katika umasikini?
Mungu alimtokea siku moja usiku na kusema Kijana umekuwa unalia sana ila mimi ndio niliua wale Ng’ombe.
Mzee akasema kwanini Mungu??? Mungu akamwambia nisingewaua wale ng’ombe yale mauti yalikuwa ni ya mkeo na mtoto wako hivyo niliyaepusha na nikaamuru mauti yale yawafike hao ng’ombe.
Mzee kusikia hayo aka nza kufurahi na kumshukuru Mungu kwa kuwaepushia kifo mkewe na mtotowake.
Funzo
· Kila kitu katika maisha hutokea kwa sababu maalumu na hautakiwi kulia au kujiona kuwa wewe una mikosi sana, wapo ambao wana matatizo zaidi ya wewe na bado hawajionyeshi .
· Unapopata tatizo tumia muda mwingi kulitafakari na kisha kutumia njia sahihi katika kulitatua ili lisijeleta madhara makubwa baadae.
· Wengi twajisahau na kuamini kila tulichonacho ni lazima kuwa nacho na kutoona umuhimu wa kumshukuru aliyetupa (MUNGU)
· Wengi hatupendani na tumekaa kimitego ili kuharibiana riziki jambo ambalo si jema
· Unapopata tatizo tumia muda mwingi kulitafakari na kisha kutumia njia sahihi katika kulitatua ili lisijeleta madhara makubwa baadae.
· Wengi twajisahau na kuamini kila tulichonacho ni lazima kuwa nacho na kutoona umuhimu wa kumshukuru aliyetupa (MUNGU)
· Wengi hatupendani na tumekaa kimitego ili kuharibiana riziki jambo ambalo si jema
TUPENDANE
share kama umeipata
0 comments: