*TAFADHALI TUMIA DAKIKA ZAKO 5 KABLA YA KULALA KUSOMA HABARI HII... NI NDEFU ILA INAUMIZA SANA*
Antonia aliajiriwa kama msichana wa kazi katika nyumba moja ya kifahari jijini mbeya na alipendwa na kila mtu katika nyumba ile kwa uhodari wa kuyatimiza majukumu yake kwa muda muafaka.
Binti huyu hakujaliwa tu uchapaji mzuri wa kazi, lakini pia alikuwa ni mrembo mwenye kuvutia kwa mtu aliyetambua kwa kuwa mazingira yake ya kazi na mavazi yake yalikuwa duni kiasi cha kuficha ule uzuri wake.
Mtoto wa pili wa baba mwenye nyumba ile aitwaye Lusungu alikuwa mwaka wa pili chuo kimoja mashuhuri jijini dar. Wakati mmoja akiwa likizo alimbaka yule dada na baada ya miezi michache dada yule aligundulika ya kuwa ana mimba.
Kwa kuwa hakuwa na jinsi zaidi ya kuwaeleza wazazi wa Lusungu kuwa kijana wao alimpa mimba baada ya kubakwa, wazee wakaona ni aibu kwa kiajna wao kufanya vile na kwa kuepusha balaa la aibu wakamfukuza binti huyo na kumpa fedha zake alizokuwa akidai na kuamua arudi zake kijijini.
Maisha yalikuwa sio rahisi kijijini kule kwani binti hakuwa na uwezo zaidi ya kuomba msaada kwa wasamaria. Hata baada ya kujifungua kila jitihada aliyojaribu kuitumia ili kupata msaada kutoka kwa wazazi wa lusungu ziliishia kuwa matatizo kwani alinususika zaidi ya mara mbili kuwekwa lupango na kuamua kukata tamaa na kuomba Mungu ampe ulinzi na nafasi ya kuupita mtihani huo.
Miaka ikapita na lusungu akawa ameshahitimu chuo na amefanikiwa kujiajiri na kuwa mfanya biashara mmoja mwenye mafanikio sana. Siku moja akawa yuko na baadhi ya ndugu zake wakiwa wanaelekea mkoani ruvuma kutoa mahali kwa ajili ya maandalizi ya harusi yake. kwa bahati mbaya walipatwa na ajali mbaya ya gari na wengi waliumia ingawa hakuna yoyote aliyepoteza maisha yake.
Baada ya matibabu yaliyochukua muda mrefu akapona na taratibu nyingine zikaendelea na baada ya hapo wakafunga harusi yao iliyofana sana na kila mtu akafurahi kwani pengine ile ajali ingeweza kuwatoa uhai wao na kweli ikawa siku ya furaha.
Ikapita miaka minne akiwa na mke wake huyo bila hata ya dalili ya kupata mtoto, mama mkwe na baadhi ya wifi wakaanza kumkalia kooni mke wa lusungu kwa tatizo la kutozaa..........
Hali ile ikamfanya yule binti atumie ujanja wa ziada alioshauriwa na rafiki yake kuwa atembee na mwanaume mwingine na kisha ampe mimba na kwa kuwa mama ndiye mwenye siri ya kujua mtoto aliyeko tumboni ni wa nani basi naye akaufuata uamuzi huo.
Baada ya muda dada yule akaanza kupata dalili za ujauzito na walipoenda kwa daktari ikaonyesha na ujauzito wa miezi miwili. Lusungu alifurahi na familia nzima ilifurahi na lusungu akawa akifanya maandalizi makubwa ya kumpokea kijana ambaye ameumiza moyo wake kwa zaidi ya miaka minne.
Siku ya kujifungua Lusungu aliwahi kwenda kumsubiria mkewe na kumpokea mwanae kama ilivyo kawaida kwa kina baba wengi wafanyavyo, hivyo akafika sehemu ya mapokezi akiwa na baadhi ya marafiki na ndugu zake wenye zawadi na nyuso za furaha.
Wakiwa wako pale mara akaingia kijana mmoja ambaye walisoma na Lusungu miaka ya nyuma na wakapotezana naye, kijana akasema kuwa alikuwa pale akimsubiri mpenzi wake ambaye alikuwa akitarajia kujifungua muda huo kwa upasuaji. wakapeana pongezi na baada ya hapo kila mtu akaendelea kuongea na marafiki zake waliofuatana wakisubiri muda wa furaha.
Mara mlango ukafunguliwa na daktari akaomba baba wa mtoto ambaye mke alikuwa akifanyiwa upasuaji aende kumwangalia mtoto, kwa maajabu wote wawili wakajikuta wakiingia chumba kimoja na wote wakaenda kwa mke wa lusungu.
Kumbe mke wa lusungu alitumia ujanja wa kutembea na yule kijana alipate mimba ya kumdanganya mme wake na kuiokoa ndoa yake kutokana na kutozaa lakini na yule kijana alipokea habari hiyo kwa furaha kwani alikuwa na ndoto za kuwa baba pia.
Kwa hasira baada ya mke kubanwa akaamua kusema ukweli kuwa , "kweli mimba ile haikuwa ya lusungu na hata mtoto huyo sio wa lusungu"
Lusungu akamfuata daktari na baada ya kufanyiwa uchunguzi ikaonyesha kuwa ile ajali aliyoipata ilisababisha asije kuzaa tena kwani iliathiri njia za uzazi za lusungu.
Wakaondoka wakiwa wamechanganyikiwa yeye na familia yake kichwani wakawa na wazo moja tu kuwa labda miujiza itokee ndio Lusungu aje kupata mtoto.
Mama wa lusungu baada ya kuhuzunika kwa muda mrefu, akalikumbuka jambo na kuwashirikisha juu ya binti yao wa kazi (Antonia)aliyewahi kulalamika kuwa alizaa na lusungu.
Ilikuwa ni habari njema na wote wakapanga safari siku iliyofuata na wakaondoka wakiwa na wazo la kwenda kumtafuta Antonia ili waweze kumchukua yule mtoto ambaye waliamini sasa kuwa ni wao ili waweze hata kufanya vipimo vya DNA na kumchukua.
Wakafanikiwa kufika pale kijijini kwa kina Antonia na kukutana na bibi wa mtoto kwani antonia alikuwa mjini akifanya kazi ili amkuze mwanae.
Baada ya kujieleza na bibi kuonyesha huzuni yake, wakaomba bibi awaruhusu waonane na mtoto kwani muda huo alikuwa akicheza na na wenzake.
Bibi akiwa na kina lusungu wakanyanyuka na kuelekea kuwaonyeha mtoto baada ya kuwasiliana na antonia, mita chache kabla ya kufika eneo la michezo wakaona kuna kundi la watu, baada ya kusogea pale hakuna aliyeamini kuwa ni ajali ya bodaboda iliyowagonga watoto wadogo wawili wakiwa wanacheza mpira na mmoja amekufa pale pale....
vilio vikaanza kuwatoka hata kabla ya kuambiwa mtoto wao amekufa kwani sura ya mtoto yule ilifanana na ile ya lusungu.
Hivyo hakukuwa na ubishi kuwa mtoto wa lusungu alikufa kwa jinsi walivyofanana na baada ya hapo wakarudi nyumbani ambako Lusungu mpaka sasa hana tena tumaini la kuwa na familia na anaumia kwa ukatili aliomfanyia Antonia.
Wiki hii Lusungu ameanza mkakati wa kutafuta mtoto kutoka katika vituo vya kulelea watoto yatima ili aweze kumfanya mwanae kwani anaumia sana kukaa bila ya kelele za watoto kama familia nyingine.
Kila kitu katika maisha yako kina maana kubwa sana mbeleni.. Jitahidi kuwa msafi wa tabia na matendo yako ya sasa kwani yana maana kubwa kwa maisha ya kesho.
Furaha yako ya sasa yaweza kuja kuwa kilio chako cha siku zijazo na huzuni yako ya sasa ikaja kugeuka na kuwa furaha.
Kamwe usimfanyie mtu kitu ambacho wewe hupendi kufanyiwa ...... kila kinachopita hurudi pia
like Tabasamu na Fuledi na kisha soma comments za watu kwa kubofya hapa
0 comments: