Sitasahau siku nilipomfumania mpenzi wangu akiwa hotelini na rafiki yangu ambaye ni zaidi ya ndugu
Sikutaka tena mtu akae na kuniambia kuhusu eti nitulie au niwe na mtu nimwitaye mpenzi wangu au mke mtarajiwa.
Hebu fikiri mtu unapigiwa simu na kuambiwa kuwa binti uliyempenda na kukaa naye kwa zaidi ya miaka mitatu na mkitarajia kuanza mipango ya kukaa wawili na mahaba tele, eti yuko hotel moja katika chumba fulani akila raha na rafiki yako wa karibu zaidi ambaye ni zaidi ya ndugu?
Na kama haitoshi umeenda na kumfumania na kwa kuwa bado unampenda unafamua umsamehe kwa kuzingatia muda ambao umekaa nae na mkijiandaa kuwa mtu na mke kuwa ungepotea bure.
Lakini pamoja na kumsamehe huko bado ndani ya wiki unakuja kugundua kuwa mpenzi wako ana mimba na yeye mwenyewe baada ya kumbana sana anakuja kuthibitisha kuwa ni mimba ya rafiki yako?????????
oooh no thanks!!! it was more than hell.........
Niliachana nae na kwa kuwa kuna vitu tulishavinunua na kuviweka kama mali zetu za kuanzia maisha na baadhi ya miradi ya pamoja nikaamua kumgawia alichostahili ili kutoa maneno kwa baadhi ya ndugu nna rafiki zake wa karibu waliojua mahusiano yetu na mali hizo.
Na kuanzia hapo nilianza kuishi maisha ya mtu mwenye stress yaani maisha ya kuwa mlevi, wanawake kwa sana yaani leo huyu kesho yule hata kama waengi walionyesha kuwa wangekuwa na mapenzi ya dhati ila nikasema NO WAY ........sitaweza amini tena mwanamke.
Nilifurahia sana kuona mwanamke akilia juu ya mimi baada ya kuachwa au kuona nimemsaliti kwani ndio ilikuwa tiba ya stress zangu na niliona kuwa kila mwanamke alihitaji kupata adhabu sawa na ile ambayo ningempa Jane ambaye alinifanyia umafia wa aina yake kwa karne hii.
Kila nilipoiona sura ya ya jane iwe mtaani au kwenye mitandao ya kijamii na pia kuona baadhi ya wanawake ambao ni mastaa wa kibongo au nje wakiruka leo na mwanaume huyu kesho na yule hasira zilizidi na nikaona hizi ndio tabia za kila mwanamke hivyo nami nikazidisha bidii ya kuchukua na kuwaacha wanawake pamoja na ushauri mzuri niliopata toka kwa marafiki lakini bado moyo uligoma kubadili msimamo na kusema lazima fuledi anyooshe adabu za hawa mabinti.
Ijumaa mmoja nikajivuta mpaka hotel moja marufu sana hapa jijini mbeya na kisha nikakaa na kuagiza pombe yangu na kuendelea kuburudika huku nikiperuzi mitandao mbalimbali ya kijamii na kujisomea baadhi ya comment za wadau wa ukurasa huu na kama ujuavyo kuna mabingwa wa kukomenti facts na wengine wanajijua wenyewe matusi kama walizaliwa hukoooo..... lakini ndio marafiki unakuwa huna jinsi tena.
Pale nilipokaa pembeni yangu alikaa dada mmoja ambaye kiukweli alionekana kuwa busy na kazi zake huku akiendelea kupata vinywaji na inaonekana kama sio kaaririwa sehemu basi alikuwa na kazi zake binafsi kwani alionekana kuwa smart na mwenye kujitambua..
Ni ule uzuri wake ndio ulio nifanya niwe nikimkodolea macho kila dakika na dakika chache ikanibidi nitulie baaada ya kuingia kundi la marafiki zake na kunifanya niwe napata taabu kumkodolea macho kutokana na kuzungukwa na wale warembo bomba lakini kila dakika niliona nazidiwa hivyo nikawa na kiburi cha kumwangaliac tu bila kujali.
Nikasema moyoni huyu leo simwachi naka haitoshi nae lazima alizwe tu kama wengine maana ule uziri wake ulikuwa wa viwango vya kuridhisha na alifaa kwa matumizi yote kama vile kwenda naye outing, kujirusha naye na hata kutambulisha kwa marafiki, wafanyakazi na bado akakodolewa mimacho na watu wenye nia mbaya na viumbe hawa kama mimi.
Uzalendo ukanishida kwani kuna mwanya ulijitokeza nikasema hapa sikosei yaani nafanya kweli kwani kuna simu iliita na akatokanje ili kuipokea kwa utulivu.
Alipotoka nje tuu kuongea na simu nami nikamfuata nikijifanya naelekea nje pia kupokea simu na kisha kumdaka na kuanza kuongea nae mambo mawili matatu lakini jambo la msingi lilikuwa ni kubadilishana mawasiliano.
Siku zikaanza kusonga mbele na tukaanza kuwa na ukaribu wa kutoana out mara kukaribishana nyumbani na nilichomshangaa ni kuwa katika kaa yangu hakuwa na tabia ya kuingilia ratiba zangu, kunishtukiza kuja home kwani kila alipotaka kuja aliniuliza kama nina muda wa kuonana nae na kama nilimwambia nipo busy alielewa hata kama nilimdanganya.
Lakini jambo la kuvutia zaidi ni kuwa hata tukitoka out naye alitamani alipe bill, akitaka kuja na marafiki aliniuliza na hakuwa mtu wa kunipekuwa wala kutaka kuongelea issue yoyote ya masuala ya ndoa mimi na hakuwa na tamaa bali alikuwa mwelewa kwa kila jambo.
Kuna mara nilimuudhi hata kwa makusudi lakini alinishangaza kwani uso wake ulikuwa na furaha na kama mabishano yangezidi angeniacha na kuondoka bila neno na kesho yake angenifuata na kuja kuyadadili au kuna wakati alinishika na kunikiss na kusema MABISHANO HAYAJENGI TUKAE NA KUTATUA NA TUWE NA MUDA WA FURAHA ZAIDI KULIKO UGOMVI..
Uuuuh!!! kidume nakuja kuzinduka tuna mahusiano ya zaidi ya mwaka na nusu na jambo zuri kuliko yote sijawahi kufikiri kumwacha na kila siku namwona mzuri na wakunivutia mwenye mapenzi moto moto zaidi ya jana.
Na ile tabia yake ya kuwa wa kwanza kuomba msamaha hata kama ningemkosea na kunisihi tuwe na maelewano pamoja na ule wepesi wake wa kunisikiliza kwa kila jambo na kunipa ushauri mzuri, vikaanza kunipa nami ujasiri wa kuomba msamaha pale nilipokosea na kupenda kuepuka kumkwaza..
Kwa kweli nikaanza kufurahia kuwa naye nikaanza kumiss uwepo wake kila mara hasa siku za weekend na nikwa na tabia ya kutoka nae, kumshirikisha mambo yangu na matatizo yangu na kwa mbaaali nikajiona napunguza unywaji taratibu na baadae kuwa natumia muda mwingi kufanya mambo ya msingi na kuwa naye na kusahau habari za kubadilisha wanawake na ule ukatili na jane akapotea akilini..
Miaka miwili ilipotimia tu nikaomba tuanze taratibu za kuishi pamoja na akanikubalia ingawa akaomba tukae chini na kufikiri tutahitaji kuja kuishi maisha ya namna gani tukiwa kama mme na mke.
Nikamwambia natamani maisha haya ya urafiki yaendelee mika yetu yote naye akaonyesha kufurahia sana tamko hilo.
Leo hii ni mwaka wa saba tangu tuoane naye na tunaishi kama tupo siku ya kwanza ya uhusiano wetu na tumekuwa tunaitana marafiki hata watoto wetu wanatufurahia kuwaa na wazazi kama sie.
Kila nikikumbuka visa vilivyopita nakaa na kusema sio wanawake wote wabaya ila wanawake wana nafasi ya kutufanya sisi tuishi vyema au vibaya.
Hadithi hii ni ya uongo ila kama unaona iko poa fuata nyayo hizo kwa kuyajenga mahusiano yako na umpendaye kuwa yenye furaha na kuepuka tabia za usaliti na pia kwa kujifunza kumpenda atakavyo na kuja kuishi mtakavyo.
kama umeelewa like Tabasamu na Fuledi na kisha soma comments za wadau bofya hapa
NA DEDICATE HII KWA YULE DEMU ALIYENIPIGA KIBUTI.......
maoni juu ya story hii whatsapp 0713317171
0 comments: