Haina jina
Kila siku itokayo kwa Mungu ilivyokuja na kutoweka na ndio utajiri wangu na heshima ilivyozidi kunitawala.
Nilimshuru Mungu sana na kuzidi kumwomba anipe baraka na hekima zaidi niweze kuishi miaka mingi nikizitumia mali hizo kwa hekima na busara.
Nilipata wakati ngumu wa kujua yupi rafiki wa kweli kwani kila mmoja alionyesha kuwa jirani zaidi na mimi akinijali kwa moyo wake wote, kweli nilifurahi.
Kubwa na lililonipa wakati mgumu zaidi ni baada ya kupendwa na mabinti watatu tofauti na mmoja aliyenipenda kwa dhati zaidi nilianza kukaa nae tena baada ya shinikizo la wazazi wangu.
Hali hii ilinipa wakati mgumu kwani kila mmoja wa watu walionizunguka walionyesha kunipenda zaidi na kuahidi wako na mimi kwa dhiki na faraja na kweli nilionja mapenzi hayo.
Nakumbuka siku moja nikiwa natoka kazini kurudi nyumbani huku niko na rafiki zangu, mara nikaanza kujisikia homa kali na kuomba nipitie duka la madawa na kupata dawa kwani nilielewa fika kuwa itakuwa homa ya uchovu kwani nilifululiza kazi bila mapumziko.
Baada ya kutoka hapo nilirudi nyumbani na kupumzika. Usiku homa ilipanda na haraka nikakimbizwa hospitalini kwangu na kupewa chumba maalumu.
Hospital hii niliijenga na kuifanya ya kisasa sana kutokana na shida za matibabu ambazo hapo awali ziliwakumba mama zetu wakati wa kujiifungua na kwa watu wengine kama mimi muda huu kama ungepata tatizo ungetakiwa utembee maili kadhaa kuipata huduma hii.
Hali ikazidi wa mbaya pale hospitali na baada ya kulazwa pale kwa siku tatu daktari akagundua kuwa nilikuwa na matatizo ya figo na nilitakiwa nibadilishiwe mara moja au lasivyo nitafariki.
Nikakaa pale hospitali zaidi ya wiki kila mmoja aliyetakiwa kunisaidia nipate figo akikimbia na kutorudi tena hospital... Mama yangu tuu na wadogo zangu walikuwa tayari kunisaidia ingawa ikaonekana damu zetu haziendani.
Binadamu alivyo wa ajabu yule mpenzi wangu pekee niliyekuwa nakaa yeye akarudi nyumani chukua fedha za kumtosha na kurudi zake kwao.
Kila mtu niliyemsikia akisema atanipenda kwa shida na raha nikaona akitoweka na wishowe kubaki mimi na wazazi wangu na marafiki wawili wakisubiri umauti wangu.
Nakumbuka jioni moja mama akasema kuna mtu anataka kunitolea figo, nikamwambia mama hilo litakuwa jema ila sasa ngoja nife tuu kwani siku zinavyozidi kwenda ndio ninavyozidi kuumia na kuona dunia na yale mapenZi ya mwazo yakinitupia kisogo.
Mama alilia na mwishowe akaniomba nimkubalie huyo binti anipe hiyo figo. Nikaruhusu aje ndani.
Ile anaingia tuu, nilishikwa na butwaa kuona ni binti ambaye niliwahi kumsaidia ada ya chuo mwaka wake wa mwisho na kumsaidia kupata ajira na wala hakuwa mpenzi wangu....nikamkaribisha.
Dada akaja na kusema, " kaka kwa msaada ule ulionisaidia naona sina namna kusema asante zaidi ya kuokoa uhai wako sasa.Niliumia sana baada ya kuambiwa unaumwa na marafiki wamekukimbia... Naomba nikusaidie sasa"
Sikuwa na cha kusema zaidi ya kumkabidhi kwa dokta fuledi na akaanza kuandaliwa ili siku ya nne tuingie chumba cha upasuaji.
Siku ilivyofika akaandaliwa na daktari akamleta chumbani kwangu na ndugu zake na wangu wakiwa wametuzunguka ili tusali na kuagana kwa mara ya mwisho kama lolote lingetokea na kupoteza uhai wetu au mmoja wetu.
Baada ya sala fupi walishangaa kuona naamka kutoka kitandani nikiwa nimeshika pete ya uchumba na ua nilivyoficha na kumwambia, "Je utakubali kuolewa na mimj?"
Hakuna aliyeamini kuwa nilifanya mchezo na dokta fuledi wa kuigiza kuumwa ili nitambue nani ni ndugu na rafiki wa kweli kwangu.
Mwezi mmoja baadae nilifanikiwa kufunga ndoa na binti yule na wiki chache wale walioanza kuniibia ofisini wakijua nitakufa walisalimisha mali zangu wengine wakipandishwa kizimbani na yule binti aliyeiba fedha baada ya kurudisha siku mbili baadae alikutwa kajinyonga kwa kuepuka fedhea na wale marafiki feki walipukutika na sasa naishi vyema na mke wangu ambaye ananipenda kwa dhati........
Wewe unayesoma acha kuamini kila kitu.....! Ila kumtambua rafiki wa dhati ukiwa kwenye furaha ni shidaaaaa.
soma comments za wadau kwa kubofya hapa
0 comments: