Hips na mwili wangu vilivyoniponza na kunipeleka kifungoni

11:06:00 Unknown 0 Comments

Mtaani kwetu hakuna aliyekuwa hanijui na kama ingetokea mtu ukamuuliza jina Mwana basi lazima angeongezea yule Mwana Mahips?????

Kiukweli mtoto nilijaliwa yaani hips hilo wowowo ndio usiseme na kugongesha magari au watu kuingia mtaroni nikiwa napita rodini ilishazoeleka machoni pangu.

Dada naomba namba yako ya simu! mara dada umeshalipiwa mara! ooooh dada una mme! na mameno kama hayo ilifikia kipindi yalizoeleka kwangu kiasi cha kuyachukia kabla ya kuanza kuyapenda tena upya.

Kila mchumba niliyekaa nae hatukumaliza mwezi na kuachana kisa wivu, eti no kusalimiana watu eti kuchati marafiki fb na hata kutoka out na kaka zangu NO!!!

Nikaanza kuuchukia uumbaji huu niliobarikiwa kwani haunipi uhuru wa kuwa na niwapendao bila wivu kujipenyeza na hatimaye kuniacha bila penzi kudumu.

Siku moja nikabahatika kumpata kijana mmoja ambaye kiukweli alionyesha kunipenda na cha kunishangaza ni jinsi alivyoweza kunipeleka hoteli tofauti za gharama kubwa na kubadilisha magari ya kifahari kama pasiwedi ya akaunti yangu ya facebook huku Umri na utajiri wake ukiwa tofauti.

Nilikula raha na mtoto wa watu na alinifurahisha kwani yeye hakuwa na wivu jambo ambalo nikajua kuwa tutaweza kaa kwa muda sasa.

Siku moja akaniambia kuna deal nataka nikupe tena wewe na utatengeneza fedha nyingi sana.

Nikamwambia nipe hun wangu wa ukweeeee.

Akaniambia deal hilo litafanyika miezi saba baadae ila kama nina uhakika wa kulifanya anaweza nipa malipo ya awali..... Nikakubali na hasa ukizingatia nilivyochapika kipindi hicho na mzee na wadogo wananitegemea kazi yangu ya usekretari majanga matupu,hivyo akaniambia siku ya pili yake nikachukue malipo ya awali nyumbani kwake.

Siku ya pili nikaenda pale na kukutana na wenzake watatu na akanitambulisha kuwa mmoja ni mhasibu na wapili ni mwanasheria na mwingine ni msaidizi wao.

Akanipa mfuko kama wa nailoni na ndani baada ya kuhesabu zililiwa milioni 20 keshi.

Nikashtuka na kusema mbona hivyo tena, akaniambia kuwa ni za kawaida na nikifanya kazi watanimalizia malipo yangu na kuwa mazuri mara mia ya haya.

Baada ya kutoka hapo nikaingia show room na kujinunulia ki lady walker (VITS) na fedha baadhi kumalizia ada za wadogo na kumtumia baba kijijini fedha za kilimo na zilizobaki nikaona nifanyie fujo mjini lakini kichwani nawaza ni biashara gani hiyooooooooooooo?????????????

Miezi ile ikasogea na siku ikafika wakaniita mpaka nyumba ile na wakaanza kuniambia kuna mzigo natakiwa kuusafirisha na utakaa mwilini mwangu.................

Akili ikaanza kusinyaaaa taratibu kabla ya kijana mmoja akiyejitambulisha kwa jina la dokta kuniambia kuwa natakiwa kuchanwa hips na makalio watoe baaadhi ya nyama na kuweka.......................................................

Comment "malizia" kwa kubofya HAPA uone yapi yalimsibu Mwana naye alijinasua au la ........Na je malipo ya awali ilikuwaje???????????????????

You Might Also Like

0 comments: