Hii nayo mpya kabisaaa: Mke mwingine aokota mayai chumbani kwake.....

10:57:00 Unknown 0 Comments

Mke alikuwa akifanya usafi nyumbani 
kwake, 

kwa bahati akakuta kibox kidogo chini ya 
mvungu wa kitanda, alipokifungua alikuta kuna 
mayai matano na shilngi milioni mbili. 
Mumewe aliporudi alimuuliza kuhusu kile kisanduku 
na mayai ni ya nini? 

Yule bwana akamjibu mkewe kwamba, alijiwekea 
utaratibu kuwa kila akitoka nje ya ndoa ananunua 
yai moja na kulihifadhi mle katika kisanduku. 
Mkewe akiwa na furaha akamwambia duh! yaani 
tangu tuoane miaka mitano iliyopita umetoka nje 
ya  ndoa mara tano tu! 

Kumbe wale walikuwa wananiambia kuwa wewe ni 
malaya sana hawakuwa sahihi ni wachonganishi 
tu... 

Mke akauliza, haya na hizi shilingi milioni mbili ni za 
nini? 

Mume: Huwa nayauza yale mayai pindi yakiwa 
mengi  na fedha naweka humo...! 

You Might Also Like

0 comments: