Kamwe naapa siji kuitumia whatapp tena yaliyonikuta siri yangu

22:23:00 Unknown 0 Comments



Niliamka mapema mida ya saa kumi na nusu za alfajiri na kisha nikaamua niutumie muda huo kuangalia kulikuwa na mpya gani mtandaoni hasa katika kipindi hiki cha kombe la dunia.

Niliwasha laptop yangu na kuanza kuperuzi habari kabla ya namba moja ngeni kunitumia text via whatsapp yenye picha nzito.

Picha hizi zilinifanya niduae kwa dakika kadhaa kwani kwenye picha alioneshwa mzee mmoja tajiri sana pale mtaani kwetu akiwa uchi na binti mmoja kigoli wa mtaa ule ambaye macho yangu yalimtambua.
Gadhabu na kisasi vilinipanda kwa kasi mithiri ya utitiri katika banda lililosahaulika la kuku wa kienyeji na kusema sasa huyu mzee kazi nitamwonesha.

Binti yule kigoli alikuwa si mwingine bali ni mwanadada Hanifa ambaye kwa kipindi hicho nilikuwa nina mahusiano naye wa zaidi ya miezi saba na pamoja na tetesi za yeye kutembea na tajiri huyo nimwitaye lofa kusambaa katika makundi mengi ya vijana lakini bado yeye alikataa katakata.

Nilijaribu tujibu text kwenye ile namba lakini ikaonyesha kama haitumiki tena whatsapp na nilipojaribu kumpigia namba ikawa haipatikani jambo lilolonifanya nitumie mbinu ya kumrushia fedha na kuona jina lake la usaliji anaitwa MWAKIBUBU MTALAKUMBOGA.

Duh, jina lilinifanya nitabasamu kiasi kwani nikaona ni kama vioja vya fuledi na kama haitoshi sijawahi sikia jina hilo hata mara moja nikaamini linaweza kuwa ni jina la kimaabara lakini nayo haikunipa shida kwani picha nilishazipata.

Asubuhi hiyo sikufikiria chochote zaidi ya kuanza kuzisambaza kwenye makundi mbalimbali whatsapp na baada ya kuridhika nikanyanyuka kwenda kuripoti kazini kwangu kwani ilikuwa ni siku yangu ya kwanza kuriport katika kazi hiyo mpya.

Nikaripoti na nikiwa kazini napewa majukumu kuna rafiki zangu wakawa wananipigia simu wakidai kuwa kuna picha chafu za Hanifa zimesambaa mtandaoni mie nikawa najifanya kama sijui vile kwani nilitumia namba ambayo sikuwahi isajili.

Saa kumi za jioni marafiki wakawa wameniita niende sehemu wanipongeze kwa kupata kazi hivyo nikafika hotel moja iitwayo TWIHIDZANGA HOTEL na kisha kuanza kupata bia nikiwa na marafiki pale.

Shamra shamra zikaendelea na wakati huo kila mtu akionyesha kufurahishwa na wengine kuchukizwa na kitendo cha Hanifa kunisaliti na zaidi baada ya tukio la picha jambo ambalo mie nikajifanya kama mgeni kulisikia na nisiyependa liongelewe.

Baada ya kitambo cha bia na vyuku aka ndege nikanyanyuka kwenda chooni na nikiwa najiandaa kumaliza kukojoa mara nikasikia sauti ikisema Bee Mwagito.

Sikutaka kugeuka nyuma mpaka pale nilipokatishwa kukojoa na kibao na nilipogeuka nilikutana na sura ya mtu mmoja ambaye sina kumbukumbu kama niliwahi kuonana naye.

Wakati huo nikawa nimejawa na hasira nikamuuliza je unataka nini?
Akasema wewe mr bee mwagito nakuita then wajifanya kiburi?
Nikadaka sio jina langu....

Nilipokea ngumi ya pili iliyonipoteza fahamu na nakuja kuzinduka nipo sehemu nisipo pajua.
Nusu saa baadae aliletwa kijana mmoja ambaye sikumtambua na baada ya muda kaka yule wa bar aliyenitweka ngumi akaja na kuniambia mr bee yaani wewe na mwenzio mnaamua kumchafua boss mtandaoni kwa picha za kutengeneza?

Wakati huo sasa nikawa nimekumbuka ile line niluyoitumia niliwahi kuisajili kwa jina la Bee Mwagito na kumbe ndiyo niliyoitumia kusambaza hizo picha na ilikuwa kwenye simu na yule kijana wa pembeni kumbe ndiye aliyezitengeneza na kunirushia picha hizo kisa yeye aliporwa hanifa na mimi na alitaka kunipa kesi ndio maana alinitumia kwa namba fake.

Nikaanza kulia na kujiona sasa ndio mwisho wangu umefika kwa kuingizwa mkenge na yule kijana nikalia zaidi kila nilipomwona na sasa tukawa tumepewa kazi ya kuzitoa mtandaoni picha zote au la sivyo tutauawa pale kwani hakuna aliyejua kiendeleacho na tupo wapi.

Tulihangaika bila mafanikio na kisha wale majamaa wakatuchukua na kutupeleka msituni ambako huko walikuwa sasa na lengo moja la kutunyonga live.

Nikalia sana tena kwa uchungu bila kujua nini chaendelea na baada ya kulia tukapandishwa kwenye kile kitanzi nikamwangalia yule kijana na kuumia kwa uchungu jinsi alivyonipa kesi feki na ujinga wa mie kukurupuka.
Hatimaye kitanzi kikawekwa na tukatundikwa shingoni na kunigwa huku wao wakiwa wanaondoka na kutokomea nami nikijitahidi kujinasua kwa kukosa pumzi huku nikipiga kelele jamani niokoeniiiii!!!! 
nakufaaaa!!!! Wameninyongaaaa!!!! simtaki tenaaaaa!!!!!! nimekosaaaaa!!!! mtaniuaaaaa!!!!!!

kwa bahati nzuri kamba ikakatika na kuanguka chini kwa kishindo kumbe niko sakafuni nikiwa nimelowa mkojo baada ya kuanguka hapa hotelini nilikofikia kutoka kitandani na kumfanya mchepuko akimbilie nje akijua nimedata kumbe ni ndoto ya asubuhi.....duuh

You Might Also Like

0 comments: