Kijana amuua rafiki yake kisa habari za udaku

19:48:00 Unknown 0 Comments

Mtafya na Nolesy ni marafiki wawili waliokuwa na kuishi wakipendana kwa dhati na kukua wakiwa marafiki jambo ambalo liliwafurahisha sana wazazi wao na marafiki waliowazunguka.

Walisoma shule pamoja, walicheza pamoja, walisali pamoja na hata kazi walipata wakati mmoja wakiwa katika mashirika tofauti.

Mtafya akawa wakwanza kuoa katika ndoa iliyofana sana. Siku moja weekend majira ya adhuhuri Nolesy akaamua aende kumtembelea rafiki yake kipenzi.

Alipofika pale akaambiwa ya kuwa Mtafya ameondoka na akapewa chai na baada ya hapo akaamua arudi zake nyumbani kwake baada ya kuongea kidogo na shemeji yake.

Mara mtafya akarudi na kumwona mkewe akiwa analia sana sana. Baada ya kudadisi akaambiwa kuwa Nolesy alikuja na kumbaka na kuondoka.

Bila neno Mtafya akatimua mbio mpaka nyumbani kwa Nolesy, Nolesy alifurahi alipomwona Mtafya akija ila furaha ikaisha pale alipogundua mfya kaja kwa shari kwani alikuwa kakasirika akiwa na chupa mkononi.

Hata bila ya kuuliza neno Mtafya akampiga Nolesy chupa ya kichwani na kumsababishia maumivu makali kwenye ubongo kabla ya kumkimbiza hosptital alikodai kuwa rafiki yake alivamiwa na majambazi.

Akarudi nyumbani haraka na kabla ya kuingia ndani akasikia sauti ya mkewe akiongea na mtu kwa njia ya simu,

" Unasikia Habiba wala usijali nimefanya kama ulivyosema na kumsingizia kuwa Nolesy kanibaka. Nafikiri sasa watakuwa wamenuniana balaa shostito wangu"

Habiba ni binti ambaye alikuwa akimpenda sana Nolesy na alishawahi kumtaka kimapenzi Mtafya pia, ila wote wakamkataa na Habiba alijua kuwa mtafya ndio anamfanya asimpate Nolesy hivyo alitaka kuwaharibia furaha yao.

Mtafya akaingia ndani bila kuongea huku akitokwa na machozi na kukimbia mbio kwenda hospital ili akaombe msamaha kwa Nolesy lakini haikuwa bahati yake kwani Nolesy alishakata roho kutokana na kujeruhiwa vibaya ubongo wake na damu nyingi kuvuja.

Mtafya alilia sana na mpaka leo hajui afanyeje ili kusamehewa kwa kumpoteza rafiki yake kipenzi wa miaka mingi.

Kila siku anajiuliza kwa nini alikuwa mjinga kiasi kile mpaka kuchukua maamuzi bila kumsikiliza rafiki yake...... Ni mara zaidi ya tatu amejaribu kujiua na kudakwa na watu.

*Ndugu yangu kumbuka shetani hutumia kila njia ili aweze kuharibu furaha zetu kila siku kwa kuwatumia watu wa karibu yetu.

*Hasira ni hasara hivyo ni bora kila wakati kuamua kufikiri jambo na kulichambua kwa kina kabla ya maamuzi yoyote yale.

Tuitumie jioni hii ya leo kutafakari juu ya mahusiano yetu na ni jinsi gani twaweza kumkwepa shetani anayetuharibia furaha zetu maishani mwetu, majumbani mwetu, makazini na mashuleni kwa kuwatumia watu wa karibu yetu.

You Might Also Like

0 comments: