Mwizi Mpumbavu Zaidi Duniani, Utamu Wa Facebook Wamkamatisha

20:04:00 Unknown 0 Comments

CBS Minnesota imeripoti habari ambayo inamhusisha mwizi ambaye polisi walimtaja kuwa mmoja kati ya wezi wapumbavu zaidi duniani, Nicholas Wig mwenye umri wa miaka 26.

Bwana Wig anadaiwa kuvamia nyumba ya mtu wakati mwenye nyumba hayupo na kuiba vitu
kadhaa lakini mwisho akagundua kuna computer yenye internet, na ndipo alipoamua kuingia Facebook kufanya yake lakini ghafla aliondoka
na kuiacha computer hiyo huku akisahau ku-log out.

Unaambiwa mwenye mali alipofika kwake alitamani kulia machozi baada ya kugundua kuwa tayari amelizwa vitu kadhaa nyumbani
kwake, lakini alipoishika computer yake iliyoachwa na mwizi huyo aligundua kuwa mwizi wake aliingia Facebook na akaondoka bila ku-log
out kwa hiyo taarifa zake na picha zake zote ziko wazi.

Baada ya kuripoti polisi, hatua za kumsaka zilianza mapema na wakafanikiwa kumkamata jamaa tena akiwa amevaa saa aliyoiba kwenye nyumba hiyo.

Mwanasheria wa County/wilaya ya Dakota, James Backstrom alipofanya mahojiano na SBC
alitamka kuwa hajawahi kupata kesi ya mwizi mpumbavu kama ya wig

You Might Also Like

0 comments: