Kisa ambacho kila nikipost marafiki huomba kirudiwe kwa kuwa kimewaokoa wengu kuhukumiwa kwenda jela

11:15:00 Unknown 0 Comments



Niliamka siku hiyo nikiwa na mwili mwepesi na kama kawaida yangu nikamshukuru Mungu kwa siku hiyo na kuanza kuandaa kifungua kinywa.

Baada ya chai, kufanya usafi wa chumba na kujiandaa mida ikawa tayari ni saa nne na robo.
Tayari nikaanza kujivuta kuelekea meza ya magazeti ili nipate kuona kuna tangazo gani la kazi niweze kuomba maaana kusaka kazi kulianza kuwa shida.

Nikiwa njiani ghafla nikapigiwa simu ya kuwa nimechaguliwa kuwa ofisa habari wa shirika fulani na kuwa jumatatu ya wiki ijayo nianze kazi na baadhi ya maekekezo yametumwa kwenye barua pepe yangu tayari.

Baada ya simu ile furaha ya ajabu isiyo na mfano ikanikumba na nikatamani kumpugia mama yangu ambaye alikuwa akikesha usiku na mchana kuniombea nipate kazi.....

Simu haikuwa na vocha ikanibidi nitembee umbali kidogo kwenda kupata salio.

Nikaiweka ile vocha na kutembea umbali fulani huku naongea mama kupitia simu na kisha kutupa ganda la vocha na kuondoka.

Ingawa wakati natupa ile vocha nilisikia sauti za watu wakibishana kuashiria kuna ugomvi mkubwa na wa hatari lakini mimi sikujali hilo kwani furaha yangu na mawazo yalitawaliwa na maongezi ya simu..
Kila mtu alifurahia sana hasa mama na mdogo wangu ambaye sasa naye aliamini ndoto yake ya kurudi shule imetimia.

Siku ya pili nilichelewa kuamka na nikiwa ndani mwangu nikasikia mlango unagongwa.
Nilipotoka nikashuhudia polisi wanne ambao walidai wana mazungumzo na mimi kituoni.
Nikaomba nifunge mlango na kuambatana nao mpaka walikopaki gari na kuondoka kuelekea kituoni.
Ndani ya lile gari kulikuwa na sura ambazo sijawahi onana nazo, ingawa hilo kwangu halikunihusu ila swali langu lilikuwa je kosa langu ni lipi au wana mazungumzo gani?????????????

Pale kituoni nikatoa maelezo juu ya siku yangu ya jana ilianzaje na na kuishaje, lakini pia nikaambiwa kuwa nahusiswa na kifo cha bwana mbeta ulasi Fitindi.

Na kuwa sehemu yalikofanyika mauaji hayo pia waliokota ganda la vocha ambayo ilingizwa kwenye simu yangu muda huo huo.

Nikaanza kuhisi kama niko ndotoni vile na kabla ya chochote nikaomba nimpigie mpenzi wangu ambaye yeye alikuwa mitaa ya karibu aje na kuweza kupeleka taarifa nyumbani kwa wazazi ambao walikuwa wakiishi mbali na mimi.

Robo saa baadae nikashangaa kuona mama na wadogo zangu na baadhi ya mjirani wanaingia pale.
Kumbe waliwahi waje nyumbani kunisapraizi kwa kupata kazi ila hawakunikuta na simu yangu inakisika ikiita ndani wakakaa pale wakinisubiri mpaka mpenzi wangu alipowakuta na kuwapa habari ya mimi kuwepo kituoni

Tukaongea nao na baada ya hapo wakanihakikishia watamtafuta mwanasheria mzuri na mimi nikawekwa mahabusu.

Usiku ulikuwa mrefu kwani nililia na kunyamaza na kisha kuanza kutafakari juu ya maisha haya mapya yasiyo na uhuru na kufikiri ni lini nitatoka nikaona hata ile bahati ya kuanza kazi ikipotea machozi yakazidi kunitoka.

Nililetewa wakili siku ya pili na siku chache baadae tukapandishwa kizimbani na wenzangu tuliohusishwa pamoja na kesi ikaahirishwa ili kupisha uchunguzi uendelee nami nikaendelea kuwepo gerezani.
Ikawa miezi sita imepita nikiwa kule gerezani nikisubiri hukumu ambayo niliamini ya kuwa ni hukumu ya kifo na kwa muda huo hali ya kutamani kurudi uraiani ilinitoka na sasa nikawa ni mtu mwenye matumaini yaliyokufa nikisubiri miujiza.

Miezi 14 baade uchunguzi ukakamilika na tukawa tunasubiri siku ya hukumu mimi na wenzangu ambao wao nao walihusishwa na tukio hili.

Siku ya hukumu nikiwa pale mahakamani sikutaka kumwangalia mama kwa jinsi nilivyoumia na kuamini ni jinsi gani atakuwa anaumia na kuhuzunika.

Nikafikri pia ndoto zetu za kuwa na miradi ya kuisaidia familia mara nitakapo pata kazi na sasa anasubiri kushuhudia mwanae akipewa hukumu ya kifo au maisha jela kuwa kamwe sitaweza kuwa nae na kutimiza ndogo zetu.

Hakimu aliingia na baada ya kupata heshima zake hukumu ikaanza ambapo kijana wa kwanza alikutwa na hatia na kupewa adhabu ya kifo, wa pili naye akapewa adhabu ya maisha jela.

Zamu yangu ilipokaribia nikaona mwanasheria wangu akiwa na uso wenye huzuni na badhi ya ndugu wakianza kulia nami kwa uchungu nikajikuta kamasi na machozi yakinitoka kabla ya kusikia nikiambiwa naachiwa huru kwani sina hatia na hakimu akagonga nyundo yake na kuondoka.

Nilipiga kelele kubwa za kumshukuru Mungu kabla ya kufinywa na mdogo wangu aliyeniamsha usingizini na kushangaa watu wakinitazama na wengine kucheka kwa chini chini.....

Kumbe muda huo wote nilikuwa nimelala kanisani wakati wa mahubiri na nikapiga kelele za kutisha pake kanisani

Niliipata aibu ya mwaka siku hiyo pale kanisani kwetu........

Whatsapp 0713317171 kwa kutangaza bure matangazo ya biashra mbalimbali katika blog hii pendwa

Soma COMMENTS hadithi hii Facebook

You Might Also Like

0 comments: