Mambo ya kustaajabisha usiyo yafahamu kuhusu wanadamu wa leo

12:38:00 Unknown 0 Comments

Mambo ya kustaajabisha usiyo yafahamu kuhusu wanadamu wa leo

Wakati wewe unatoa mimba, kuna mtu anasaka mimba kwa miaka kumi bila mafanikio

Wakati wewe kijana una mkataa binti uliyempa mimba, kuna mzee ana miaka nenda rudi akiwa anakesha akiomba Mungu amjalie mtoto

Wakati wewe una inyanyasa familia yako leo, kumbuka kuna mtu anatamani apewe familia na aipende

Wakati wewe unaichukia kazi uliyonayo, kuna mtu ana vyeti vyake safi ila hajawahi kupata
kazi ya aina yoyoye na anaishia kwenye interview tuu

Wakati wewe unawadharau na kuwasahau wazazi wako bila kuwajali. Kuna watu wanalia
usiku kucha na kuumia kuwakosa wazazi

Kumbuka, hakuna maisha yoyote zaidi ya haya na huna budi kuwa na shukrani kwa kile
unachojaliwa sasa....

Pia ni bora kuwa na mpangilio wa maisha ukimtanguliza MUNGU na
kushukuru kila ulichonacho na kufurahia nyakati ulizonazo

You Might Also Like

0 comments: