MFAHAMU MTANZANIA WA KWANZA KUWA BILIONEA HUKO ZIMBABWE

10:52:00 Unknown 0 Comments


Jamaa alitoka bongo na kwenda kufanya kazi huko nchini Zimbabwe katika kampuni moja
maarufu ya kuchimba madini.

Baada ya kukaa kwa muda mrefu akaamua arudi bongo ili aje kusalimia ndugu, jamaa na marafiki
kwani aliwakummbuka sana.

Kwenye basi alilokuwa akisafiria akaibiwa baadhi ya mizigo na baada ya kwenda katika ofisi zao
wakamlipa na kumpa dola bilioni 10 za kizimbabwe.

Jamaa akadata na kuanza kupiga simu bongo kuwa wamfanyie mautundu ili apate kiwanja
maeneo ya kifahari ajenge nyumba na akaanza kuuliza ni jinsi gani anaweza kununua hisa katika
kampuni ya Bakharesa na kununua magari ya kifahari.

Kama haitoshi akaanza kuwapigia vijana wa kazi wazee wa Serengeti anunue vogu moja matata sana na waisafirishe mpaka hapa bongo.

Alifurahi akijua kuwa zile dola akizibadilisha zingekuwa ni hela nyingi sana za kibongo nyingi za kitanzania.
Kufika pale tunduma akaingia bank ili azibadilishe na kuziweka kwenye akaunti yake kwani akahofia usalama wake na hela hizo atakapo taka kuanza safari ya bongo.

Jamaa kidogo azimie kuona zile dola bilioni kadhaa zimegeuka na kuwa elfu sabini za kitanzania
kwani fedha ya zimbabwe imeshuka thamani.

Mpaka sasa jamaa anaumwa vidonda vya tumbo kwani haamini kuwa ndoto ya viwanja na
nyumba imeyoyoma.

Unampa ushauri gani kijana wetu?

You Might Also Like

0 comments: