NENO USILOTAKIWA KULIKOSA JUMAPILI HII "Kupitia dirisha akachungulia na kuona mwanamke yule akiwa anaoga"................ unajua nini kilifuata??????? Soma

10:30:00 Unknown 0 Comments


Siku moja mfalme Daudi akiwa katika moja ya vyumba vyake kupitia dirishani alimwona mwanamke mmoja nyumba jirani akiwa anaoga.

Daudi akampenda sana na kuwatuma watumishi wake wakatafute habari zake nao waliporudi wakamwambia kuwa yule ni Bath-sheba mke wa Uria ambaye ni jemadari wa vikosi vya israel.

Mfalme Daudi akaomba binti yule apelekwe katika jumba la kifalme na akalala naye.Baada ya siku kadhaa yule binti akapeleka ujumbe kwa mfalme Daudi kuwa alikuwa na mimba yake.

Daudi akapeleka ujumbe kwa mkuu wa vikosi vilivyokuwa vitani Yoab kuwa amwambie Uria arudi mara moja. Uria akafika na baada ya kuulizwa hali ya vita mfalme Daudi akampa baadhi ya zawadi na kumruhusu aende nyumbani akijua angelala na mkewe na mimba ikawa yake.

Asubuhi akashangaa baada ya kuamka na kuambiwa Uria na watu wake hawakwenda majumbani mwao ila walilala mlangoni pake.

Mfalme akamwita Uria na kumuuliza kwa nini hukwenda kulala kwako? Naye akajibu kuwa kamwe nisingeweza kwenda kulala na kufurahi nyumbani wakati kuna watu wako vitani wakiumia.

Wakalala pale na siku ya pili Uria akaondoka kurudi vitani bila kwenda kwake na ndipo mfalme Daudi akatuma ujumbe kwa yoab kuwa uria apangwe mstari wa mbele kwenye mashambulizi makali na kisha wenzake wamwache apigwe hadi kufa.

Yoab akafanya hivyo na baada ya muda wa maombolezo ya kifo cha Uria kwisha, Daudi akamchukua Bath-sheba na kumfanya mke wake ndani ya jumba lake na akamzalia mtoto.

Mungu akamtuma Nathan na kumwambia Daudi, “Palikuwa na wanaume wawili waliokuwa katika jiji moja, mmoja alikuwa tajiri na yule mwingine alikuwa maskini.

Yule mwanamume tajiri alikuwa na kondoo na ng’ombe wengi sana; lakini yule mwanamume maskini hakuwa na chochote isipokuwa mwana-kondoo jike mmoja, aliye mdogo, ambaye alikuwa amenunua.

Naye alikuwa akimhifadhi hai, na huyo kondoo alikuwa akikua pamoja naye na wanawe, wote pamoja. Kondoo huyo alikuwa akila tonge lake, na kunywa kutoka katika kikombe chake, naye alikuwa akilala kifuani pake, na kondoo huyo akawa kama binti kwake.

Baada ya muda, mgeni akaja kwa yule mwanamume tajiri, lakini hakuchukua kutoka kati ya kondoo zake na ng’ombe zake ili kumwandalia yule msafiri aliyekuja kwake. Kwa hiyo akachukua yule mwana-kondoo jike wa yule mwanamume maskini, akamwandalia yule mtu aliyekuja kwake.”

Ndipo hasira ya Daudi ikamwakia sana yule mwanamume, naye akamwambia Nathani: “Kama Yehova anavyoishi, mtu huyo aliyefanya hivyo anastahili kufa Na kuhusu yule mwana-kondoo jike, atamlipa mara nne, kwa sababu yeye amefanya jambo hili na kwa sababu hakuwa na huruma.”
Ndipo Nathani akamwambia Daudi: “Wewe mwenyewe ndiye yule mwanamume!
Basi Daudi akamwambia Nathani: “Nimemtendea Mungu dhambi.” Kwa hiyo Nathani akamwambia Daudi: “Yehova naye ameacha dhambi yako ipite. Hutakufa. Ingawa hivyo, kwa kuwa bila shaka hukumheshimu Yehova kwa jambo hili, pia yule mwana, uliyemzaa, atakufa hakika. Kisha Nathani akaenda zake nyumbani kwake.
Na Mungu akampiga yule mtoto ambaye mke wa Uria alikuwa amemzalia Daudi, akawa mgonjwa.
Mfaleme daudi akafunga akilala chini na kumwomba Mungu amponye yule mtoto huku akilia na hata wafanyakazi wake walipotaka kumnyanyua yeye alikataa akiendelea kuomba kwa siku kadhaa.
Siku moja watumishi wake wakawa wananong'onezana jinsi ya kumwambia daudi kuwa mtoto yule amekufa. Wakasema kama wakati akiwa hai aliomboleza vile itakuaje kusikia amekufa?
Daudi akagundua wakiwa wananong'onezana akawauliza amekufa? wakajibu ndio... ndipo akanyanyuka na kwenda kuoga, akavaa mavazi mapya , akaenda nyumba ya bwana kusujudu na kisha akaomba aletewe mkate wale watumishi wakashangaa na kumuuliza,
“Ni nini maana ya jambo hili ambalo umefanya? Ulifunga na ulikuwa ukimlilia mtoto alipokuwa hai; na mara tu mtoto alipokufa ukasimama, ukaanza kula mkate.”
Daudi akajibu, “Nilifunga, nikawa nikilia mtoto alipokuwa bado hai, kwa sababu nilisema,
‘Ni nani anayejua kama Yehova huenda akanipa kibali, na hakika mtoto aishi?’ Sasa kwa kuwa amekufa, kwa nini nifunge?
Je, ninaweza kumrudisha tena? Mimi nitakwenda kwake, lakini yeye hatarudi kwangu.”
Na Daudi akaanza kumfariji Bath-sheba mke wake. Na zaidi ya hayo, akaingia kwake, akalala naye. Baada ya muda akazaa mwana, naye akaitwa jina lake Sulemani. Na Yehova akampenda mwana huyo. Basi akamtuma Nathani na kumwita jina lake Yedidia, kwa ajili ya Yehova.
Funzo
*Hakuna kitu kibaya kama tamaa ya kutaka kutamani mali isiyo yako na kuichukua kwa hila kama mfalme daudi alivyoweza mpokonya mke wa uria na kisha kuamuru Uria awekwe mstari wa mbele katika mapigano ili afe
*Mungu akiamua kukuumbua huwezi jificha hebu fikiri jinsi Daudi alivyoamua kutumia ujanja wa kumrudisha Uria ili alale na mkewe na mimba ionekane yake lakini bado ikashindikana na pia jinsi alivyomtuma Nathani na kwenda kumpa daudi mfano uliogua tukio lake
*Mungu pia huchukizwa na dhami za tamaa kama alivyoweza kumadhibu daudi na kumuua yule mtoto
*Kwa kula anguko ni muhimu sana kumrudia mungu wako kama vile daudi alivyolitambua kosa lake na kisha kuomba msamha kwa Mungu wake wa kweli
*Ni vizuri kuacha mambo yapite na kutoyakumbuka kama vile mfalme daudi baada ya mtoto kufa alivyosahau na kuanza maisha mapya na kisha kuja kupata mtoto sulemani ambaye pia Mungu alipendezwa naye na baadae alikuja kuwa mfalme mwenye hekima
Ni vyema tuutumie mfano huu wa Daudi kusahihisha maisha yetu na jinsi tunavyoishi na jamii inayotuzunguka na matendo yetu kwao.

Jumapili njema

You Might Also Like

0 comments: