Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu nilichoweza.
Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu nilichoweza.
Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao.
Akanenepa!! Penzi letu likawa huru alipo anza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi. Alinifundisha.
Nikaegemeza maisha yangu yote kwake.Akanifanya nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake.
Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume
wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae?
wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae?
Nilimkubalia kila kitu.Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu. Kweli nilikuwa.msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu.
Nilipenda tututmie kinga lakini aliipinga sana. Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani nikafanyaalivyotaka. Kwa mara ya kwanza nikatoa mimba. Haikuniuma sana!!
Niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na.atanifichia aibu hii.
Nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga.
Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai. Tayari aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua.
Pombe kidogo na nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa nawahi kulewa. Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo baya lililonifanya niandike haya kwako. Akaniingilia kinyume na maumbile.
Alinilawiti!!
Nilishindwa kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume
asiyejulikana hata kwa wazazi. Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala.
Najuta kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu.
Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona katika kioo ukatoweka, simu za mara
kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu. Hakutaka niende kwake.
kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu. Hakutaka niende kwake.
Wakati huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na maumbile.
Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha
nabakimwenyewe katika msoto. Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema
nini mimi?
Ninajua alishindwa kusema neno moja tu. Tuachane!! Nilijua tayari ameniacha!!!
Afya yangu ikadolola sana, nikalazimikakwenda kupima hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia. Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali
sana.
sana.
Nikaanza kumsahau yule aliyenitenda..Nilipomaliza chuo akajitambulisha nyumbani na
alitaka kunioa. Akanioa kweli.
alitaka kunioa. Akanioa kweli.
Maisha yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba. Mume wangu alikuwa mvumilivu sana, hakuwa hi kunilaumu.
Lakini niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali. Nikaambiwa kizazi change kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya kinyume na maumbile yamenivuruga kabisa.
Nililia sana huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu. Dunia haikuwa mahali
pangu sahihi.
pangu sahihi.
Nimekuandikia barua hii mdogo wangu.Uisome mwenyewe!! Lakini uwasimulie wengi baada ya kifo changu. Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyika na kufanya mambo magumu kuwaridhisha wapenzi wao.
Waambie watakufa kwa mateso kama mimi. Wasipokusikiliz a usijisikie vibaya maana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mumemdanganyifu. Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!
Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi.
Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku moja ya kuwafikishia wasichana
hawa.
hawa.
Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume mwenzako AMENITENDA HIVI!!!
soma majibu hapa
0 comments: