Duuuh kwa ushirikina huuu tutaishi mbeya kweli?????? Hapana ngoja nianze kufikiri kuhamia mikoa iliyotulia kama sumbawanga

07:02:00 Unknown 0 Comments




Evaristo na Salva ni marafiki waliodumu kwa  zaidi ya miaka kumi wakifanya biashara zao kwa pamoja huku wakifurahia mahusiano yao kikazi na maisha ya kawaida.

Walianzia maisha yao mkoani mbeya na kisha kuhamia jijini Dar baaada ya kuona huko kuna nafasi kubwa ya kuzifanikisha biashara zao ili waweze kukua zaidi.

Jijini dar wakafanikiwa kufungua ofisi yao na kuendeleza kazi zao kwa ushirikiano mkubwa sana huku wakigawana vyema mapato yao kwa wakati muafaka na kufanikisha mipango yao pia.

Siku moja wakafanikiwa kufanya kazi moja kubwa na ikawapa fedha za kitanzania keshi milioni 72 ambazo walitakiwa kugawana sawa sawa yaani kila mmoja kupata milion 36.

Fedha hizo akatumwa akazichukue Salva ambaye alifanikiwa kuzichukua lakini akiwa njiani kwa kuwa fedha hizo zilikuwa kwenye mfuko akaamua kuzima simu na kupotea zake.

Siku zikazidi kuyoyoma bila ya Salva kupatikana na kutokana na upelelezi wa Evaristo akafanikiwa kupata taarifa kuwa Salva yupo jijini Arusha akiwa amejificha na kufanikiwa kupata namba yake.

Baada ya kupata namba yake akampigia Salva na kumsihi ampe mgao wake na waachane ili kila mmoja aendelee na mambo yake bila kudhuriana jambo ambalo Salva hakutaka kulifanyia kazi.

Evaristo baada ya kuona hivyo akafunga ofisi yake Dar na kurudi zake kwao huko mbeya na kisha kusafiri mpaka kijiji kimoja ndani huko na kukutana na mganga mmoja anayesifika pale kwa tiba za kishirikina.

Baada ya kufika pale na kumwelezea mganga yule wa kienyeji mkasa mzima, mganga akamwambia unataka nimfanyeje huyo rafiki yako? Evaristo akasema mpe adhabu ambayo atanitafuta na kuja kuniletea fedha zangu.

Mganga akamwambia sasa nenda na hii nazi utaipasulia njia panda na kisha utatamka deni lako mara tatu na kuondoka pale haraka bila kuonekana na mambo yataanza kuwa mambo.

Evaristo akaondoka na kwenda kufanya kama aliyoagizwa na mganga wake na kisha akaizima simu yake na kubadili namba kabisa na kuhamishia makazi yake jijini Mbeya.

Wiki moja baadae Salva akaanza kuvimba tumbo huku akitokwa na vitu vyenye mfano wa fedha mdomoni huku akilalamika kuwa niliiba fedha za rafiki yangu zaidi ya milioni 40 ambazo zilitakiwa kuwa mgao wake.

Kila siku ilivyozidi kwenda tumbo lilizidi kujaa na akilalamika kwa maumivu na hata alipopelekwa hospitali aliambiwa hili swala ni la kishirikina apelekwe kwa wataalamu wa kienyeji wakamalize, amlipe mwenye fedha zake au waende akaombewe.

Kanisani akaogopa kwa kuwa alijua ni dhuluma ikabidi ndugu wakae na kuanza kufikiri jinsi ya kumpata Evaristo ambaye hakujulikana aliko mpaka pale walipopata fununu za kuwa yuko mbeya na kumfuata.

Walifanikiwa kumkuta Evaristo na baaada ya maongezi machache wakakubaliana muda huo huo kumlipa fedha zake bank baada ya kufanikiwa kuchukua chache alizobaki nazo Salva kwani alitumia kwa starehe na matanuzi pale jijini Arusha na nyingine zilitokana na michango ya ndugu.

Baada ya kuhakikisha fedha zipo kwenye akaunti yake,  Evaristo akawaomba warudi dar na hali ya mgonjwa wao itabadilika mara moja watakapowasili dar.

Wageni walipoondoka Evaristo akampigia yule babu wake na kumwambia sasa amwachie jamaa kwa kuwa ameshalipwa na baada ya hapo akakaa kama siku mbili na kuwapigia simu ndugu wa Salva nao wakamshukuru kuwa sasa kijana wao tumbo limepungua na halalamiki tena kuhusu maumivu yoyote wala kutoa vile vitu kama fedha na kutamka yale maneno.

Jambo lililonishangaza wakati Evaristo anataka kulipa fedha za ujira wa yule mganga, mganga alikataa na kusema amnunulie kitu apeleke yeye huwa hapokei fedha. Evaristo akamnunulia mganga yule godoro na kumkabidhi kisha akarudi kuendelea na kazi zake.

Habari hii ya uongo hata mimi wakati naitunga imenifanya niogope kudhulumu.

Niambie kuhusu wewe umeionaje hii?




You Might Also Like

0 comments: