Njia rahisi ya kumpiga mkwara boss wako jumatatu hii

09:17:00 Unknown 0 Comments

Jamaa alikosea ofisini kupiga simu na kumpigia simu bosi wake kwa bahati mbaya akiwa na dhumuni la kumpigia mfanyakazi mwenzake ili amzingue....

Jamaa: "Oya we mpuuzi lete chai vikombe viwili haraka mezani kwangu na chapati 3..!!!"

Bosi: "Hivi unajua unaongea na nani??!"

Jamaa: Acha upuuzi dogo fanya kama ulivyoambiwa lete chai fasta

Bosi: eti Hivi unajua unaongea na nani??!

Jamaa: (Baada ya kugundua kampigia bisi wake akaa kimya....)
Bosi: "Nauliza hivi... Unajua unaongea na nani??!"

Jamaa (Kwa kuzuga ikabidi tu ajibu...): "Hapana..."
Bosi: "Mimi ni bosi wako humu ndani..."

Jamaa (Akakaza sauti na yeye): "Hivi na wewe unajua unaongea na nai??!"
Bosi: "Hapana, nani wewe?!"

Jamaa(Kwafuraha zaidi): "Daaaaah, asante MUNGU!!!!"
Then akakata simu!!!!!

You Might Also Like

0 comments: