X-Mas ya ajabu kutokea katika maisha yangu

04:47:00 Unknown 0 Comments

Nusu saa kabla ya kwenda kanisani kuhudhuria ibada ya mkesha wa X-Mas akikuja bibi mmoja ambaye sijawahi kumwona maishani.

Bibi huyu aliomba tumsaidie chakula na kuwapia angependa ajumuike nasi katika ibada ya
mkesha na kuwa amefanya hivyo kwani siku hiyo alikosa magari ya kurudi kijijini kwao kwanihakuwa na nauli.

Nikaingia chumbani na mke wangu nakumwambia,tutafanyaje kuokoa jahazi hilo?

Kwani X-MAS hii imekuja wakati ambao kwanzamaisha yametubana sana na mambo mengine ndani ya nyumba ni siri yetu jinsi tuishivyo.

Kwa moyo mmoja tukakubali kumpa akiba yetu ya 30,000 kama nauli ya kumpeleka mpakakijijini kwake na pia tukajumuika wote katika ibada ya usiku ule.

Tulishangazwa na jinsi bibi yule bibi alivyokuwa mchangamfu na mwenye kutushauri jinsi yakuwa na busara na ushirikiano katika kuijenga familia bora.

Zaidi alijigusia suala la kutokata tama walakutegemea kulipwa fadhila kila unapotoamsaada.

Wakati anaondoka siku ya pili yaani leo asubuhiakanipa zawadi ya kitambaa kizuri chenye maua
na mke wangu akapewa mtandio.

Zawadi hizi zikanikumbusha maumivuniliyoyapata mwaka mmoja uliopita siku kama ya
leo nipofiwa na dada mmoja ambaye nilikutananae akiomba msaada wa fedha za kutibiwa
saratani ya matiti.

Na baada ya vita ngumu ya kuupigania uhaiwake alikufa mikononi mwangu na kuniachia
mwanae mmoja niwe baba mlezi na zawadikama alizoniachia bibi huyu.

Zawadi hizi na kumbukumbu hii zilinifanya niliekwa uchungu nikimkimbuka dada yule na baada
ya fikra hizo nikapitiwa na usingizi kabla ya mkewangu kuniamsha na kuniambia nina mgeni.

Mgeni huyu kaja kunipa taarifa ya kuanza kazirasmi january 19 mwakani.

Kazi hii mimi na mke wangu tumeipigania tangumwaka jana na mpaka sasa naamini ni Mungu
ananipa mafanikio kupitia dada yule aliyenifiamikononi mwangu.

Mungu awabariki wote mnaofanya matendomema kwa watu wote, na mzidi kupata barakakila siku kwa kadri mwombavyo.

You Might Also Like

0 comments: