Yaani mpaka kombe la dunia limalizike ndoa nyingi zitakuwa gereji

14:13:00 Unknown 0 Comments

Jamaa yuko home kwake  anaangalia mpira, mke wake akamfuata sebuleni:

Mume wangu hiyo taa hapo mlangoni haiwaki vizuri, itengeneze basi.

Jamaa akajibu: Nitengeneza taa wakati naangalia mpira?
Hivi unaniona nafanana na mafundi umeme?

Mke akanyamaza.

Baada ya dakika chache akamfuata tena:

Mume wangu hivi umeona meza imevunjika mguu mmoja kule
jikoni?


Jaribu basi kuitengeneza.

Jamaa akamcheki halafu akajibu:

Hivi we mwanamke una nini?

Ukiniangalia nafanana na mafundi seremala?

Mke akaguna halafu akaondoka.

Baada ya muda akarudi tena:

Baba watoto, hapo kwenye ngazi mlangoni umeona tofali moja limetoka?

Jaribu basi kulirudishia.

Jamaa kwa hasira akajibu:

Hivi hupendi kuona mtu amekaa kwa starehe?
Mimi nafanana na mafundi ujenzi?

Baada ya kuona anasumbuliwa jamaa akaamua aende zake kuangalia mpira baa.

Akiwa anacheki mpira nafsi ikamsuta kwamba alichomfanyia mkewe si kizuri akaamua kurudi home kumuomba msamaha.

Alipofika akukuta tofali mlangoni limetengenezwa, meza jikoni nayo imetengenezwa na hata taa mlangoni nayo imeshatengenezwa, akashangaa akamuuliza mkewe vipi?

Mkewe akajibu:

Alikuja msugaule yule kaka wa nyumba ya jirani akanisaidia ila kwa masharti kwamba, nimtengenezee ice cream au nikalale kwake lisaa limoja.

Jamaa akajibu:

Msugaule  mjinga kweli, kwa hiyo ukamtengenezea hiyo ice cream?

Mke ajibu:

Kwani mimi nafanana na kiwanda cha bakhresa?

You Might Also Like

0 comments: