Bado watanzania waendelea kutamba kimataifa kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kukutumia fursa hata nyakati hatarishi

15:51:00 Unknown 0 Comments

Mtanzania, Mnyarwanda, na Mkenya walikamatwa kwa kuzamia nchini China.

Wakaambiwa adhabu ni mbili kifo au adhabu nyingine ambayo wakiishindwa pia wanauawa. Wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.

Wakapelekwa msituni wakaambiwa waingie msituni kila mmoja kwa njia yake halafu kila mmoja arudi na matunda 10 ya kufanana. Wakaingia msituni kila mtu njia yake.

 Mnyarwanda akarudi wa kwanza. Karudi na ma apple 10. Akaambiwa adhabu ni kumeza yote mazima mazima moja baada ya jingine bila kufunga macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa! Akamezaa kwanza. Safi. Kumeza la pili akashindwa kuvumilia akafunga macho. Akapigwa risasi akafa. Wa pili Mkenya akaja ana Straberry 10. Akaambiwa masharti. Akaanza kula bila kufunga macho wala kulia wala nini. Alipofika cha 9 akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.

 Wakiwa kuzimu Mnyarwanda akamuuliza Mkenya.. "Vipi wewe mbona ulishindwa kuvumilia wakati ulibakisha tunda kimoja tu?" 

Mkenya akajibu: "Kaka, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mtanzania anakuja na matikiti maji 10

You Might Also Like

0 comments: