Ila madaktari nao wana visa nyakati fulani....
Kuna jamaa yangu alipata jibu moja matata sehemu ambayo huwa haitajwi kirahisi rahisi.
Hosp tukafika jama yupo chumba cha upasuaji, kaja dada mmoja mzuri balaa na ni jirani na jamaa alishatupaga ndoano zake hazikunasa.
Jamaa kala ngumu kasema hapasuliwi mtu hapa niitie dokta.
Dokta kaja ni rafiki na jamaa pia akamuuliza " mgonjwa nasikia unagoma matibabu?"
Jamaa kasema mie namsubiri daktari sasa wananiletea huyu dada ananiambia nishushe suruali haya sio maadili.
Daktari kasema huyo ndio mtaalamu jamaa ikabidi awe mpole yule binti afanye yake na tuondoke.
Jamaa anadai ni mwezi wa sita sasa anaogopa kupita mitaa ya kwao kukiwa kweupe anaona soni kuoana na yule dada dokta....

0 comments: