Dada zetu kila usaliti mnaotufanyia malipo huwa hapa hapa duniani... kama huamini soma

20:32:00 Unknown 0 Comments


Mimba ilikua na ikiwa imesalia miezi michache kujifungua kabla ya mimba ile kutoka, jambo lililomfanya maria azidi kuchanganyikiwa kwani ilikuwa ni mimba yake ya tatu katika ndoa yake na kijana aitwaye Nolesy ambayo ilidumu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.

Bila huruma Nolesy alimfukuza Maria na kuamua kutafuta mke mwingine akiona kama Maria ana mikosi ya kwao. Maria akarudi mtaani na kupanga nyumba yake na kuendelea kuishi. 

Haukupita mwaka kwa kuwa alikuwa na kazi nzuri na kila kitu katika maisha yake akaanza kuona anahisi kuwa anahitaji kuwa na mwenza. Wakati anafikiri hivyo tayari alikuwa na urafiki na kijana mmoja aitwaye Mtafya ambaye walishaanza kufahamina nae kwa wakati huo.

Taratibu wakaanza kuona dalili za kupendana na mambo yakazidi kuwa mambo mpaka yule kijana alipomwomba Maria wafunge ndoa. Maandalizi yakaanza na kicheni pati ikafanyika zikiwa zimesalia siku mbili wafunge harusi kijana Mtafya akatokomea mitini na baadhi ya fedha za michango.

Maria alihuzunika kwa muda na baada ya hapo akasahau na kuendelea na maisha yake kama kawaida na kusema sasa hataki mwanaume. Wiki, miezi mara mwaka, akiwa kanisani katika kikundi cha kwaya alipoamua kuutumia Muda wa zaida kumwimbia bwana Mungu wake, akakutana na kijana mmoja mwimbaji aitwaye Trio.

Trio kwa muda mfupi alimbadilisha mawazo na kumfanya Maria aamini tena katika mapenzi hasa akimfariji kwa kila kilichotokea. 

Mahusiano yalianza kwa kasi lakini baada ya miaka miwili baadae waliachana na Trio kwa shinikizo kutoka kwa wifi zake kwani hawakumpenda wakimwita mzee na kuwa amechoka hata kama umri wake haukuwa mkubwa lakini sababu zilikuwa nyingi.

Maria akaapa na kusema kamwe hataolewa tena ila kwa wakati huu ila atamtafuta mtu wazae nae na alee mtoto peke yake. Wakakutana na kijana aitwaye Gachi ambaye yeye ikambidi ampende Maria kwa kuwa alikuwa akimhonga hela ili wazae nae lakini jitihada hazikufanikiwa baada ya dokta kugundua ya kuwa Gachi alishaumwa sana na gono na lilishaharibu kizazi chake.

Maisha yakazidi kuwa magumu kwa maria na kuona sasa kama kila kitu kinakuwa msumari wa moto katika maisha yake hasa ndani ya mapenzi. Akanuia kuokoka kabisa na kujikabidhi kwa Mungu lakini shetani akampitia kupitia mzee wa kanisa aitwae Sai na wakaanza mahusiano na miezi mitatu baadae akawa mjamzito ingawa maajabu ni kwamba mimba ile ikawa imetungwa nje ya mji wa uzazi wakaitoa.

Baada ya hapo akaambiwa hatakiwi kushika mimba tena kutokana na tatizo katika mji wake wa uzazi. Jambo lile lilimuumiza kichwa sana na kumfanya aanze kudhohofika na baadae ndugu wakamshauri aende kwa mzee mmoja mwenye hekima na busara pale mtaani aliyekuwa akishauri watu aweze kumshauri.

Katika mahojiano yule mzee alimwambia Maria amwambie ukweli kuhusu maisha yake na dhambi anazofikiri alizifanya maishani pasipo kuogopa. 

Maria alimwambia yule mzee, " baba ni kweli sikuwa mwema, nilitoa sana mimba tangia sekondari, chuoni na hata nilipoanza maisha. 

Niilikuwa nikiwasaliti wapenzi wangu na kuna mmoja alifikia kuwa kichaa baada ya mimi kumkataa asinioe pamoja na kuwa tulikaa miaka mingi kwa pamoja.

Sio hayo tu, pia nilikuwa nagombanisha kila marafiki zangu kwa kutembea na wapenzi wao na hata wake wa kaka zangu sikuwapenda kwani kila mara nilikuwa mgomvi na kuonyesha hawastaili kuishi na kaka zangu.

Na tukio la mwisho nilimsingizia rafiki yangu kwa mpenzi wake kuwa alikuwa mhuni na kutumia waganga ili kumteka mpenzi wake na wakaachana na siku chache mimi nikawa na yule mzee na wakati huo rafiki yangu alikuwa na ujauzito wa yule mzee akashia kutaabika"

Mzee akamjibu.

Mwanangu, Najua umewahi kusikia kuhusu jehanamu.

Lakini jehanamu ya kwanza huanzia hapa hapa duniani. 

Mtu hulipwa makosa yake akiwa hapa hapa duniani, yaani kwa mfano:

*Kama ulisaliti jua utasalitiwa tu siku moja na kuumia pia
*Kama ulimdanganya mpenzi wako jua nawe utadanganywa
*Kama uliwachukia mawifi zako nawe jua utaolewa na kuona chungu
*Kama ulitoa mimba kuna kipindi utahitaji kuwa na watoto na unaweza ukakosa na kuumia
*Kama ulichukua waume wa wenzio nawe tegemea kuna siku utatendewa ubaya.
* Hata kwa wenye majungu na fitina majumbani, makazini na mtaani huwa tunashuhudia wanavyokuja kuumbuka

Kwa kifupi mwanangu maisha ni sawa na kuokota pesa na kupoteza.. kwamba kama utaokota pesa jua kuna siku itapotea tu. 

Hivyo kwa kila baya ufanyalo hapa duniani malipo na majuto huanzia hapa hapa cha msingi hapa ni kuanza kuwaomba msamaha uliowakosea na Mungu wako.

Binti yule aliondoka akiwa kainamisha kichwa chini huku analia na kuanza kuwatafuta wale wote aliowakosea ingawa hakufanikiwa kuwapata wote na wengine alishawasahau.

Unajifunza nini juu ya mlolongo huu? 























You Might Also Like

0 comments: