Duh demu wa chuo mbeya anisababishia majanga tena... kazini hapakaliki na nyumbani haparudiki

18:16:00 Unknown 0 Comments



Mimi sio mpenzi sana wa kukaa nyumbani hasa mida ya jioni maana huwa nikitoka kazini ni moja kwa moja kupata bia na kutembelea washkaji.

Hivi majuzi nilipata bahati ya kukopeshwa verosa na ofisi yetu kwa hiyo kwa wiki ya kwanza nikaanza kuonja utamu wa kutembea ukiwa umekaa... acha tuu asikuambie mtu .

Niliwahi kusikia kuwa ukiwa na usafiri basi kila binti ni wako tena bila kukunja goti wamdaka mithili ya kumbi kumbi.

Basi kila nikitoka ofisini  ratiba ikabadilika mara nijifanye naenda TIA, Mzube Garden, TEKU yaani kila chuo kilichopo hapa mbeya mjini ilimradi niweze kutana na penzi la kichuo yenye kila aina ya majina matamu hasa watakapo pesa, mfano swty, swiry, hun, han, darl pal na mengine mengi ambayo wewe msomaji nawe huwa unamwibia mpenzi wako.

Nikawa nimefanikiwa kudaka wawili wa tatu na kujiona mjanja sana yaani. Juzi jioni nikiwa narudi nyumbani, nyumba ya nne kabla ya kufika kwangu  nakutana na bonge la toto nikapunguza mwendo na kushusha kioo taratibu huku mziki ukitweta ala za kijana Ali Kiba akinikumbusha kuwa "Mapenzi yana  run dunia"

Mtoto akaniambia yeye anakaa na dada yake na pia anasoma Mzumbe, duh nikamwambia plz chukua kadi yangu na tafadhali kesho nicheki ukiwa free na tukaachana.

Siku ya pili yake akaniendea hewani nami kwa sifa nikawasha mchuma na kumpeleka sehemu moja maarufu sana mtoto akapata lunch, kisha nikamfungulia waleti nakumpa maneno ya kiutu uzima, ukiambiwa maneno jua ni mshiko tuuuu.....

Kweli mtoto akaanza kunipotezea usikivu si kazini wala nyumbani kila muda mimi na whatsapp mara dia nipigie picha unafanya nini,mara kashanitumia picha mara sijui nini.... mweeee mapenzi ya digitali usiyafananishe na yale ya enzi za posta na simu... kwanza sitaki kukumbuka.

Jana mtoto nikamchukua tena mida ya saa nane na akanisindikiza lunch na nilikuwa sina haraka ya kuomba penzi kwani alishaniahidi kuwa weekend nitamchukua na kuwa nae siku nzima nami nyumbani nilishampanga wife kuwa weekend nitaenda kuwatembelea wakulima fulani ambao wanataka kuniuzia mashamba ya miti kwa hiyo akawa hana noma kabisa kazi ikawa ni kwangu.

Leo asubuhi nikawa nimechelewa kutoka home na wife alishawahi kwenda kazini nami nikaamka na kwenda kuoga nimemaliza kuvaa ile nachukua laptop zimeanguka picha tano zinaonyesha mimi nikiwa na yule demu huku namlisha chakula na kukumbatiana pale mzumbe gardeni

Hapa nimedata na wife jana usiku alikuwa mchangamfu kama kawaida yake na wala hakuonyesha dalili ya kitu chochote na mbaya zaidi kashaenda kazini.

Hata hamu ya kwenda kazini imekata na sijui nifanyaje na ni kwa vipi kapata picha au yule binti alikuwa ni mtego wa kuninasa au sijui ni nini?????????????

I hate girl oooow eeeeeeh am dying ... maana na wife ni mbabe hapa hata nyumbani sijui nirudi au lah sijui akija jioni itakuaje, au  gari nikafiche maana asije vunja vioo duuh.

Duh

You Might Also Like

0 comments: