Ha ha ha ha duuh kazi ipo: Video ya H BABA yagharimu Laki Na Nusu.
Pamekuwa na uwekezaji mkubwa kwenye video za bongo hivi karibuni na takriban wasanii wote wakubwa wamejaribu kutumia mamilioni ya pesa kwenye video bora na kuzifanya na watayarishaji wa nje.
Msanii wa muziki wa bolingo bongo fleva H Baba amebana matumizi zaidi kwenye video yake mpya ambayo anasema imegharimu 150,000.
H Baba ameandika facebook “ Video yangu imetumia 150,000 laki na nusu, namshukuru Mungu nimemaliza salama. Video yangu sio ya mamilioni, kaa mkao wa kula uwone laki na nusu ilivyofanya kazi Jiandae pia na filamu mpya kuingia kambini.
H Baba anasema video amepewa ofa yani video ya bure na director Saimako.
From: sammisago.com

0 comments: