HABARI HII IMENIFANYA NIAMINI KUWA MUNGU NI MUWEZA WA YOTE
Anna alihitimu chuo na kukaa nyumbani kwa zaidi ya miezi saba akisaka ajira bila mafanikio na kuishia kula chakula cha baba na mama bila mwelekeo wowote ule.
Wazazi walimfari na kusema kuwa daima mambo mazuri huja kwa wakati wake kama vile mvua ambavyo huja kwa wakati na wakati mwingine huchelwa na watu huzisubiri kwa hamu kwa ajili ya kunyeshea mazao yao shambani lakini muda ukifika huja.
Siku moja akiwa anajisomea kitabu kimoja akapata wazo moja zuri la tamsha ambalo litakuwa la kila mwaka kuhusu kuinua vipaji vua waandishi wa hadithi fupi kama hii ya fuledi na kisha kuwapa zawadi na kuzichapisha hadithi hizo katika kitabu cha pamoja na huku zikitengenezewa michezo ya kuigiza endelevu.
Baada ya kulifikiria wazo lile akarudi nyumbani na kuliandika kabla ya kuamua kumshirikisha rafiki yake wa karibu ili waweze kufanya pamoja kulihariri na kuanza kutafuta wadhamini ili tamasha hilo liweze kuasisiwa na ku likifanyika.
Kweli wakalihariri na kisha wakawa wamemaliza na kufikiri ni kwa namna gani wangeweza kuanza kupata msaada wa kuyafikia makampuni hayo na kupewa huo udhamini.
Wakamtafuta rafiki yao mmoja aliyekuwa akifanya kazi katika kampuni fulani ya matangazo na kumpa lile wazo. Jamaa baaada ya kuona uzuri na fedha zitakazotokea kupitia wazo lile akaamua kuwazunguka na kujifanya yeye ndio mwenye wazo na kuanza kuwapiga kalenda Anna na rafiki yake.
Walifuatilia na kukatishwa tamaa kutokana na majibu mabovu na baadae kuachana na wazo hilo na kuendelea na jitihada za kutafuta kazi kwani kujiajiri wakaona kama wamekosea njia.
Kwa upande wa pili rafiki yule akawa amelichukua wazo lile na kulipeleka katika kampuni moja kubwa na maarufu ya vinywaji baridi ambao wakawa wamelisoma pale na kusema watalijadili na kumpigia kwakua ni wazo zuri sana na kampuni ile ilikusudia kuinua vipaji vya wasanii kama njia ya kuisaidia jamii na kuishukuru kwa kuvipenda vinywaji vya kampuni hiyo.
Siku moja majira ya saa nane mchana Anna akiwa amejipumzisha nje ya nyumba yake akijisomea habari za tabasamu na fuledi akapigiwa simu na dada mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa kampuni ya vinywaji baridi na kuwa anamwomba kwa mazungumzo siku ya pili yake.
Asubuhi ya siku ya pili Anna bila kujua ni mazungumzo gani alikuwa akiitiwa kule aliwasili pale na akapokelewa na kupelekwa kwa mkurugenzi wa kampuni ile ambaye alimwambia jinsi walivyopenda wazo lile na kuwa wao watakuwa wafadhili wakuu na kwamba maandalizi yaanze kwani kwa kuanzia watampa msaada wa kusajili kampuni yake na kuwa mradi huo utakuwa ukigharimu shilingi za kitanzania milioni 350 kwa kuanzia.
Mpaka sasa yule rafiki aliyetaka kuwadhulumu lile wazo hajui ni nini kimetokea kwani Anna na mwenzake wanaendelea vyema kampuni yao Ambayo inazidi kukua na kupata wafadhili wapya kila kukicha na kuajiri vijana wengi wenye vipaji huku mamia ya watu wenye vipaji wakinufaika kila mwaka kwa kuinuliwa kazi zao.
Lakini ukweli ni kwamba wakati yule kijana analiiba lile wazo na kulipeleka katika ile kampuni alibadilisha sehemu nyingi ila akasahau sehemu moja mhimu iliyoonyesha msimamizi mkuu wa mradi huo ni nani?
Mungu akisema ndio hata atokee shetani wa aina gani hawezi badili kwa kuwa ni wakati wako
Hivyo kila mara amini kuwa pamoja na mapito yako na kudhulumiwa haki zako Mungu yuko upande wako daima.Na kama unahitaji kuona shuhuda mbalimbali soma katika ukurasa wangu wa facebook
0 comments: