Kwa mtindo huu mpya jamani ndoa zitakuwepo kweli????????????????

09:35:00 Unknown 0 Comments





FOMU YA MAOMBI YA KUMUOA BINTI YANGU KIJANA, JAZA FOMU HII KWA MWANDIKO WAKO MWENYEWE NA KWA HERUFI
KUBWA. 

Mimi ......................., natuma ombi la kumuoa binti yako.

Nina umri wa miaka .............. 

TAFADHALI JIBU MASWALI YAFUATAYO KWA UAMINIFU. 

1. Huwa unahudhuria ibada? Ndiyo/Hapana

2. Una Masters au PhD? Ndiyo/Hapana

3. Una undugu au urafiki na tajiri yeyote mkubwa mjini?Ndiyo/Hapana

4. Mshahara wako una tarakimu 7? Ndiyo/Hapana

5. Unamiliki nyumba? Ndiyo/Hapana

6. Una gari? Ndiyo/Hapana

KAMA KATIKA MASWALI 6 HAPO JUU KUNA LOLOTE UMEJIBU HAPANA BASI USIENDELEE KUJAZA FOMU HII NA FUTA NDOTO ZA KUMUOA BINTI YANGU. KAMA MAJIBU YAKO YOTE NI NDIYO ENDELEA KUJAZA FOMU.

1. Kwa kutumia maneno yasiyopungua 50 elezea hasara za kuchepuka katika ndoa. --------------------------------------
------------------------------------------------------------
----------------------

2. Kwa kutumia mchoro elezea namna gani unaweza kuwapa heshima baba na mama mkwe wako.

3. Mfano mkeo akikwambia "Mume wangu nahitaji hela
ya kwenda saluni" utamjibu vipi? ----------------------------------------------------------------------------------------------

4. Elezea sababu 10 za ndoa nyingi kuvunjika.

5. Elezea maana ya maneno "mume mwema" kama
unavyoyafahamu wewe binafsi.

6. Wazazi wako wamefunga ndoa? Ndiyo/Hapana.
Kama ndiyo, ndoa yao ina muda gani? Kama umri wa ndoa ya
wazazi wako ni mdogo kuliko umri wako elezea kwa
nini ulizaliwa nje ya ndoa.

7. Elezea maana ya "Mume wangu urudi nyumbani mapema" kwa maneno yasiyopungua 100.

8. Toa sababu 3 ambazo zinaweza kumfanya mwanaume asilale nyumbani kwake na mkewe.

9. Ndoa ikivunjika, unadhani nani mmiliki wa watoto kati
ya baba na mama.

JIBU MASWALI HAYA KWA KUANDIKA NDIYO AU HAPANA.

1. Unakunywa pombe?

2. Unavuta sigara?

3. Una hasira za karibu karibu?

HII NI SEHEMU YA MWISHO LAKINI MUHIMU KAMA NYINGINE ZOTE HAPO JUU

1. Lini uko tayari kuja kwangu kufanyiwa intaviu? ----------------------------------------

2. Siku na muda gani unadhani ni sawa kumuhoji baba au mlezi wako wa kiume kuhusu hii nia yako? -----------------------------------------

3. Siku na muda gani unadhani ni sawa kumuhoji mama au mlezi wako wa kike kuhusu hii nia yako? -----------------------------------------

4. Siku na muda gani unadhani ni sawa kumuhoji kiongozi wako wa kidini kuhusu hii nia yako? -----------------------------------------

5. Tafadhali bandika picha yako ya rangi ya siku za karibuni ambayo itarushwa katika magazeti na mitandao ya kijamii ili kujua kama una wapenzi wengine au la.

Weka sahihi hapa: -------------------------

Rudia kuweka sahihi hapa: ----------------------------------

Asante kwa kuonyesha nia ya kumuoa binti yangu. Muda wa kupitia maombi yako ni miezi 6. Utajulishwa kama tu utafanikiwa.

Niandikie anuani zako hapa chini ili niweze kukufikia kama nitakuwa na maswali zaidi.

E-mail: _________________

Simu: __________________

Facebook: _______________

WhatsApp: ______________

Twitter: _________________

Instagram: _______________

LinkedIn: _________________

BBM PIN: ________________

Skype:__________

Kwa mtindo huu wangapi wangeoa au kuolewa?? Hebu share na marafiki nao waone hii.

You Might Also Like

0 comments: