Habari ya kuhuzunisha ya binti wa kitanzania!!!!!!!!!! "Ilidibidi niuze pete ya ndoa na baadhi ya vitu nipate fedha ya kumpeleka mtoto shule....Kama haitoshi nikaanza kutembea na wanaume nipate pesa za kujikimu"

09:08:00 Unknown 0 Comments



Mimi niliolewa na tukawa tunakaa kwetu ambako tumepanga na baadae mme akasema tuhamie kwao, tukaja kuhamia kwao yaani ukweni na kazi ndo ikaanza hapo.


Chuki baina yangu na mme na wifi na mama mkwe ikawa juu yangu mpaka nikaachika kwa mme chanzo ni mama yake anampenda sana mtoto wake wa kiume.

Sasa huyo mama hata mtoto wake akija kwangu hamuachii anakuja nae tena anakaa nae mbele kwenye gari, na hata aje kumuona mtoto wake mama yupo pembeni na hanisalimii mpaka nimuanze yeye na anaitikia basi tu na mme wangu anampenda sana mama yake na hasikii la mwingine.

Mme wangu ni mfanyakazi na tumeachana nae kwa shinikizo la mama na wifi zangu, alinipeleka mahakamani kisa hakieleweki anadai talaka anipe na ni ndoa ya kikiristo na mahakama ikatoa talaka ingawa mwanaume alihonga hela.

Sasa akawa hatumi chochote cha mtoto mpaka nikampeleka mahakamani ndo akaanza kutoa kisa kapata majimama yenye hela zao ndio anatanua mjini na gari za kuhogwa wala hakumbuki tulipotoka na nilivyomvumilia.

Mama mkwe ndio mke mwenza kwakweli yeye na mimi ni chui na paka sielewi kwann? akisikia mtoto wake anakuja kwangu anaacha safari zake ili aje nae.

Nahitaji ushauri mme kakamatwa sana na mama sijui kuna nini?

Mpaka kuna wakati mme anaogopa kulala na mie au kucheka na mie akiwepo mama na dada zake.Mara mama ndio awe anamtayarishia kila kitu nami nipo, mme wangu ndo anayemtuma mama anataka nini? 

Halafu mama na mtoto wanafanya siri kwa ndugu wasijue wanachonifanyia na ndugu wanasikia tu wakiulizwa wanasema mimi ndio na matatizo ningekuwa na matatizo si ningeitwa na kanisa au wakubwa waseme matatizo yangu??

Kikubwa mama wa mme wangu anasema nimwache mwanae ale raha na kapewa gari na mwanamke wenye hela wao ndio wanafurahia.

Yaani huyo mama ni balaa anasema hakuna mwanamke atakayemjua zaidi ya yeye na mtoto wake wa kiume na anasema hakuna mwanamke anayemfahamu kama mama yake ngoma iyo umeiona.

Mme wangu namsikiliza sana mama yake hasikii la yeyote, mimi nadhani tatizo langu kwa mme wangu lilikuwa kupekua simu zake na kukutana na wanawake tofauti kitu hicho alikuwa hakipendi ndio kosa langu nami nilikuwa nafanya sababu ni wivu na mapenzi kwa mme wangu .

Kwani nilikuwa mwaminifu katika ndoa sana tuu, Fuledi mpaka hii leo Mungu ndio anajua maumivu niliyoyapata ni umaarufu tu wa kazi zake ndio mwanaume anaanza kukudharau tena anakutamkia kuna wanawake wa maana wananitaka wenye hela zao.

Mbaya zaidi aliniacha na mtoto katika msiba wa baba yangu tulipoenda kumzika baba yangu yeye akaniacha na mtoto na kurudi zake dar ndio kimoja na alikuwa hajui lolote juu ya mtoto hata salamu hata kupiga simu.

Ni zaidi ya mwaka mmoja na nusu mtoto kaja kumuona wiki iliyopita ni Mungu tu ndio kamleta tena alikuja na mama yake na hawakufika nyumbani kwetu waliishia barabarani.

Hali ilikuwa ngumu sana kwangu sina kazi aliniachishaga kipindi sana ndio nimepigana mahakamani mpaka hela za mtoto na matunzo zimepatikana.

Nilikuwa sina msaada wa mtu yeyote hata mama yangu mzazi aliniacha hata ndugu nikawa peke yangu napigania haki ya mwanangu nilimwita Mungu nikamuuliza nimekukosea nini?

Niliuza pete ya ndoa nikauza vitu vyangu mtoto aende shule na mtoto akaenda ndio kaanza la kwanza sasa ndio mme huyo kaanza kuhudumia kwa amri ya mahakama,huyo ni mwanaume wa aina gani?

Hivyo ni vidogo nilivumilia sana niliyotendewa ni makubwa na yenye machungu kaka ni afadhali kieleweke nilimkosea nini mme au ma mkwe au mawifi lakini hakuna ni chuki ninashidwa mpaka leo hii kujua nini.

Nimesota kaka peke yangu na Mungu tu ndio kaniongoza nauza hata nguo zangu nipate nauli ya kwenda mahakamani na ya kutafutia kazi si mchezo namshukuru Mungu kaka.

Ikabidi nianze kuwa sasa na wanaume ili nipate chochote kaka maana hali ilikuwa ngumu baadae nikaacha na kuokoka Mungu nimemuona kaka kwa sasa nimeokoka nina story ndefu ata kutunga kitabu na nimesamehe lakini mama mkwe na wote walionitendea mungu atalipa.

Mwanaume huyo ndio anatanua na wanawake na kubadili magari ya wanawake starehe mtindo mmoja,nimeumia sana nikikumbuka tulikotoka chuo wote tukaa wote tukazaa ndio tukaja kufunga ndoa leo hii eti mie mwanamke gani nimemroga eti ndio niolewe nae.

Mara mie mzee mambo mengi ya kashfa mara asema mtoto kaniachia zawadi mara dada yake aseme kaka yake ana watoto kibao mara siwezi kurudiana na kaka yake labda awe kazaliwa na mama mwingine nimetukanwa sana kaka roho inaniuma .

Nimemfikisha hapo alipo wanakula wengine naumia sana kila nikikumbuka kaka .

Naomba nisiendeleee maana nahisi kuishiwa nguvu nitaendelea kukusimulia …………………….

Naomba kama kuna mtu anaweza nipa ushauri wa nini cha kufanya kwa sasa

Like Tabasamu na Fuledi


You Might Also Like

0 comments: