Harakati za kutafuta maisha zinavyoweza kupoteza maisha

18:07:00 Unknown 0 Comments



Fred na mkewe walihangaika kupata mtoto kwa zaidi ya miaka kumi bila mafanikio yoyote yale na baadae wakafanikiwa kumpata mtoto mmoja wa kiume.

Mtoto huyu alikuwa ni kama Tanzanite machoni mwa wazazi wake na kila mmoja alimpenda sana na kumpa upendo wa dhati.

Siku moja asubuhi mtoto alivyokuwa na miaka miwili na baba akiwa anajiandaa kwenda kazini, akaona chupa ya dawa baridi za binadamu ikiwa wazi na kumwomba mkewe aifunge na kuihifadhi kabatini na yeye akawahi kazini.

Mkewe akabanwa na kazi za jikoni na huku mtoto akaamka na kuona ile chupa iko wazi akavutiwa na rangi ya ile dawa na kuinywa kwa kiwango kikubwa.

Dawa ile ilikuwa ni sumu kama ingenyweka kwa kiwango kikubwa zaidi ya dozi ya kawaida kwa watu wazima lakini mtoto yule akawa ameimaliza.

Mtoto alianguka na kuzimia na kisha mama kumbeba na kimkimbiza hospital na kwa bahati mbaya mtoto yule alikuwa njiani kabla ya kuwasili kwa daktari akafariki.

Mama yule alijawa na uoga na hofu hasa akazingatia kuwa alifanya makosa kwa kutoiweka ile chupa sehemu salama kama mme alivyosema, hivyo akaogopa baada ya kuambiwa mme anakuja.

Mme alipofika kwa sauti ya upole huku machozi yakimtoka akamwambia mkewe, "Mpenzi usiwe na hofu nipo nawe"

Baba aliona hakuna haja ya kubishana juu ya nani apewe lawama kwani hayo yasingemrejesha mtoto zaidi ya kuongeza simamzi na akafikiri ya kuwa kama naye asubuhi ile angeiweka vyema ile chupa basi mtoto yule asigeweza kufikwa na mkasa huo.

Hivyo aliona kuwa alihitaji muda wa kumliwaza mkewe zaidi kuliko kumzidishia maumivu ya mawazo na simanzi kwani naye alikuwa na kosa pia.

Funzo

Kuna nyakati tunatumia muda mwingi kuwalaumu watu au kulaumiana kwa mambo ambayo hata sisi tumechangia kwa kiasi kikubwa kutoke au twatumia muda mwingi kwenye mambo mengine na kusahau kuwa pia twahitaji kuishi na kupenda uhai tulio nao


You Might Also Like

0 comments: