Haya ndio madhara ya kutokuwa makini na matumizi ya facebook
Jamani mimi nasema facebook ni upuuuzi na sitaki tena yaani kila mtu nimemchukia.Fuledi mimi ni mtumiaji mzuri wa facebook na hasa ukurasa wako lakini nasema kama sitapata mawazo mazuri kutoka kwa marafiki zako ninao waheshimu kwa ushauri bora kila mada iwekwapo mezani achilia mbali wale mamluki wanaonigia na kuharibu mjadala basi leo nitafunga ukurasa wangu na kutafuta mtandao mwingine wenye busara.
Mimi ni mfanyakazi wa taasisi fulani inayohusika na matangazo na mimi ni pia meneja wa habari pale ambaye ndio msemaji wa hiyo taasisi.
juzi nikatoka ofisini baada ya kuwa na hitilafu za umeme nikaenda kufanyia kazi internet cafe na baada ya kumaliza kazi nikarudi ofisini na kufunga milango na kwenda kupata moja baridi.
Nikaanza kushangazwa na sms nyingi toka kwenye namba ngeni wakidai mimi hapa nakupenda, mara mbona hujasema siku nyingi kama huo ndio mchezo wako na mbaya zaidi kuna baba mmoja akanipigia simu na kusema uko wapi nikufuate?
Nimauuliza una nini anasema kama ulivyoandika wewe,. nikaona ngoja nimwelekeze nilipo alipofika naona ni baba mmoja wa kisomali ameanza kunikalia kimapenzi na mbaya zaidi anaanza kuniambia tuondoke basi… Nilimlipua na ngumi moja na kisha akaondoka na wakati huo meseji zinaendelea kumiminika kwangu..
Mbaya zaidi mke wangu akanipigia simu huku akilia na kusema yaani kumbe unafanya upuuzi huo na kujianika nitauficha wapi uso wangu mimi na akakata simu, nikiwa sijui nini kinaendelea akanipigia swahiba wangu na kuniambia kaka mambo gani hayo tena?????????????
Nikamwomba anieleweshe akasema wewe soma upuuzi wako ulioandika fesibuku…. Nikawa sina simu ya kuingilia mtandaoni nikawasha gari na kwenda kutafuta net nikiwa nimepanic nasijui nini kinaendelea baada ya hapo boss akanipigia simu na kusema nakuomba asubuhi ofisini kwa nini unaiabisha taasisi hii?
Akili ikasimama nikafika net umeme ukakatika kabla ya kufanya kitu, wazo likanijia nimpigie mdogo wangu mmoja anayekaa jirani pale nilipokuwa aniletee laptop na modem.
Sikuamini nilichokiona facebook eti nimeandika “ Mamboz!!!! Nahitaji mme wa kunipa joto la maisha nimechoka kupritendi… I need my man now”
Inbox kulikuwa na text kama elfu moja na kitu na notifications ndio usiseme. Meseji nyingi za kunitusi, kunishangaa na wengine wakinitaka laivu na wengine ni marafiki zangu huwezi amini walivyo mashetani wakosa haya……….
Nikaifuta ile post na kuomba msamaha na wachache wamenilewa ingawa usumbufu bado upo kwa baaadhi ya wapuuzi na ofisini wameanza kunitania wananiita anti fesibuku.
Naombeni ushauri nianyeje ili wajue mimi ni mwanaume na sihitaji mme, nilisahau tu kulogout akaunti yangu na mtu akaandika ujinga huu pale net nilipoenda mwanzoni?????
I hate this
0 comments: