" Hellow Darling siku yako imeishaje, nimekumis sana na baridi hii hope utajilinda?..... Ila mbona kama ni namba ngeni??????

16:30:00 Unknown 0 Comments



Kama miezi miwili hivi iliyopita nilikuwa zangu katika mihangaiko yangu nje ya jiji la mbeya.

Usiku mmoja majira ya saa nne na nusu nikiwa chumba cha kulala wageni simu ikaita mie nikajua ni waif labda anataka kunitakiwa usiku mwema kwani nilikuwa sijaongea nae muda huo.

Kucheki nikaona ni namba ngeni,  huwa sina mazoea ya kupokea namba ngeni ila nikasema ngoja nipokee pengine ni wenyeji wangu wa eneo lile.

Duu!! Ikatokea sauti moja laini sana ya kike tena inaonyesha alikuwa anajiandaa kulala na anataka kuongea na mpenzi wake zile chati kama wewe unayesoma unazopenda kuongea na mpenzi wako kwenye simu... usijifanye kama hujui...

Basi nikapokea na kabla sijaongea neno akaanza " Hellow Darling siku yako imeishaje, nimekumis sana na baridi hii hope utajilinda?"

Muda huo nikawa nashangaa maana sina kazi za nje kwa muda tangu nilipooa many years ago. Basi nikaona hapa nisijifanye kuuliza jina lake wala anataka kuongea na nani nami nikaanza kula naye sahani moja.

Aiseee yule binti ana sauti yaani dunia nzima, basi tukaongea kama nusu saa na tukaachana huku yeye akilala na mie nikiwa sasa nawaza huyu binti ni wa wapi na anataka nini kwangu au katumwa kupata data kutoka kwangu na waif.

Usiku ule sikupata jibu na asubuhi nilipotaka kumpigia simu ikawa haipatikni. Nikaendelea na kazi zangu na ilipofika usiku mida ile ile simu ikaita tena na sasa nikaongea nae kwa muda mrefu zaidi ya jana yake.

Tuliendelea kuongea kwa siku kadhaa mara nikarudi zangu home na kila ilipofika mida ile ya kuongea nikajifanya natoka kwenda kupata bia moja kumbe ili niisikie ile sauti ya binti wa kwenye simu ambaye hata jina naogopa kumuuliza kwani inaonkena twafahamiana na mie naelewa kuwa ni WRONG namba.

Binti alikuwa mtata na kuwakati unaweza washa TV bila kutarajia hasa sauti na utaalamu wa maneno utafikiri ana kiwanda cha kuchapisha maneno matamu ya mapenzi mdomoni mwake.

Siku moja jioni mida ileile nikiwa najiandaa kupokea simu............................................................................................................................... Itaendelea

kama unahihitaji kupitia email/whatsapp au inbox nitext kupitia whatsapp 0713317171

You Might Also Like

0 comments: