Hiki ndio kipimo bora cha mapenzi
Katika kijiji kimoja walipata kutokea wanandoa wawili ambao walipendana sana kuliko kawaida na kuwa familia bora na ya mfano kwa jinsi wanavyopeana mahaba ya dhati kwa uhuru.
Wanandoa hao walikuwa wakila pamoja, kuongozana barabarani pamoja na walikuwa mfano kwa jinsi walivyokuwa wakweli kwao na kwa jamii..
Kila mwanamke alitamani kumpata mme wa mfano ule hali kadhalika kila mwanaume alitamani kuwa na binti mwenye heshima na mapendo ya kweli kama ya mama yule.
Miaka michache baadae baba yule akaanza kuumwa na homa ikaonekana kumfanya mama adhohofike na kutokuwa na amani kwani hakulala akikesha akimuuguza mmewe na kumpa huduma bora akishirikiana na ndugu jamaa na madaktari wa hospital alipolazwa.
Mama hakupata hata dakika ya kukiancha kitanda cha mgonjwa huku akiishiwa nguvu na hatimaye akaombwa aende kupumzika nyumbani kwani kiafya haikuwa sahihi kukaa kwa muda ule bila mapunziko ingawa aligoma mpaka pale alipolazimishwa.
Muda mfupi tu baada ya kuondoka mama yule pale hospital, huku nyuma mme wake akafariki dunia.Ndugu wakashindwa kwa muda fulani njia ipi sahihi waitumie kumwambia mama kuwa mmewe amefariki.
Baada ya mama kuambiwa alizimia kwa masaa kadhaa na baada ya maandalizi ya mazishi kukamilika watu wakatoa heshima zao za mwisho wakaenda kwenye mazishi ingawa mama yule alisindikizwa na kina mama wanne waliomshika kumsaidia kutembea kwa kuwa hakuwa na nguvu za kutembea akimlilia mme wake kipenzi.
Wakati kaburi linafukiwa mama yule alikuwa akilia na zaidi ya mara nne akafanya majaribio ya kujitupia kaburini akiomba azikwe na mmewe.
Kelele za mama kutaka kuzikwa na mmewe zikamfanya mzee mmoja mwenye hekima pale kijijini kuomba aongee kidogo.
Mzee akaanza kwa kusema, "kwa jinsi mama huyu na mmewe walivyoishi kwa kupendana hapa kijijini, kila mtu ni shahidi kuwa mama huyu akibaki peke yake bila kuzikwa na mmewe anaweza asikae hata usiku mmoja kwani hata weza. Hivyo naomba azikwe tuu pamoja na mmewe....Asanteni"
Kabla hata yule mzee hajamaliza kusema neno "asante", yule mama alikimbia baada ya kuwasukuma wale kina mama wa nne na kwenda kujificha nyumbani na hakuonekana mpaka alipohakikisha mmewe kazikwa kabisa ili wasije mzika nae.
Watu wakashangaa mama kapata nguvu wapi na kwa nini kabadili msimamo wake wa kufa na mmewe.
Usicheze na kifo bwana
0 comments: