KUNA WATU WANAIBIWA KWA DIZAINI HII MITANDAONI

07:36:00 Unknown 0 Comments



Juzi kuna jamaa yangu kupitia akaunti yake ya fesibuku akatangaza kuwa analiuza gari lake.
Basi akapigiwa simu nyingi sana na watu kibao wakitaka kununua gari hilo.

Akanipigia simu usiku na kuniambia kuwa kesho yake tuonane asubuhi na mapema yaani jana kwani kampata dada mmoja anataka kulinunua gari hilo hivyo nimsindikize akamwonyeshe na niwe shahidi wauziane.

Nikamtania sasa ndugu kama shahidi utanipa asilimia ngapi?

Akaniambia usijali fuledi wewe twende gari likitoka una laki tatu zako hapa za haraka si wajua tena mjini mpipango na wenye kuiweka mipango ni sisi?

Basi jana mida ya saa nne akanifuata nyumbani na tukaondoka kwenda kuuza gari wakati huo mie nimewaambia nyumbani waandae maji ya kunyonyolea kuku kwani nilijua haitachukua hata saa gari litakuwa nimeuzika kwani ni jipya na mie nilijua nitapokea ka hela kangu ka ushahidi plus hamu ya kuku safari ikaanza.

Tukaondoka na tukiwa njiani yule dada akawa ameshatupigia simu zaidi ya mara nne vile mpaka mie nikaanza kumlaumu rafiki yangu kwa kuchelewa ili tumwahi mteja.

Akatuelekeza alipo na hatimaye tukafika bar moja na kukutana na dada mmoja aliyeonekana ni mishentown sana.

Kumwonyesha gari akasema hili ni bonge la gari na wakalitesti na jamaa yangu wakati huo kashatuagazia bia moja moja na supu.

Baada ya kulikagua na kuridhika akamwambia jamaa kuna mteja amabye ni mme wa yule dada anakuja pale na yeye huwa malipo anafanya moja kwa moja kwa nia ya mtandao hivyo yeye anahitaji laki tano tu ya kumleta mteja hivyo rafiki ajue kama ataiseti kwenye bei au lah.

Saa moja baadae akaja jamaa mmoja ambaye alidaiwa kuwa mteja wakaliangalia gari naye akaridhika sana na wakaanza kuulizia kadi ya gari tukamwonesha akaridhika na kutupa round za bia pale tukisuribi sasa wafanye mambo tusepe.

Baada ya kula pale jamaa akatoa wazo waondoke na rafiki mwenye gari wakalipe bank na wakija iwe ni kuandikishana tu.

Mie nikatoa wazo ni vyema tumwite na mwite au twende kwa wakili, jamaa akadai poa poa ni wazo zuri na akaomba mie na mkewe tubaki tuendelee kunywa bia na kuagiza tutakacho.

Wakiwa wanataka kutoka yule mama akamwita rafiki yangu mwenye gari na kumwambia kwa kuwa wewe unaenda kulipwa huko basi nipe changu hapa hapa. 

Jamaa akajikaguaa wee akawa na laki mbili na nusu cash ambayo alitakiwa kumlipa mdeni wake mmoja, mimi nikamwambia jamaa unajua nilitoka haraka home hivyo sina wala kwenye simu na hata hivyo simu yenye miamala iko home.

Basi mama akasema,  "plz nakuamini ukiniletea uhuni utahama mjini"

Kisha akamwambia nitumie ya juu kwenye laini yangu ya simu na jamaa wakaondoka mie na mama tukabaki pale tukila bia na mie naletewa naweka kinywani tu.

Robo saa baadae yule dada akatoka  na kwenda kuongea na simu nami nikaendelea kunywa wakati huo nawasiliana na rafiki yangu anasema kampa jamaa namba ya account na jamaa yupo bank ndani anafanya mambo.

Masaa yakafika mawili sioni dalili za yule dada kuja na jamaa yangu naye anasema yule mnunuzi naye hajatoka bank labda foleni ndefu.

Machale yakanicheza nikamwambia jamaa aingie ndani..... kuingia ndani hakuna dalili za mtu.
Na mie wakati huo natala kutoka pale nilasikwa shati nadaiwa bili za vinywaji  ambazo zilishafikia 160,000.

Nikashangaa sana na kuuliza wale wenye bar mbona sie tulipewa ofa pale na wenyeji wetu?????
Jamaa wakadai kuwa waliambiwa kuna watu wanakuja kulipa na hata yule dada wakati anaondoka alidai kuwa mimi ndio mlipaji?

Nikampigia jamaa yangu akaniambia ngoja aende home kwake akachukue kadi ya bank aje tulipe na iwe SIRI YETU.

Nami kwa hasira na uchovu na kuishiwa nguvu baada ya kuambiwa wale wateja ni mara yao ya kwanza kuonekana  pale na walikiwa wakiongelea kupata nauli ya kusafiri, basi nikalala pale usingizi mzito kabla ya kushtuka mida ya saa kumi na mbili na nusu na kugundua ni ndoto za jioni kwani nililala usingizi mzito baada ya chakula cha mchana.

Ila cha ajabu nikaingia jikoni na nikakutana na supu ya kuku kumbe kweli nilipotoka kwenye mishe nilirudi na kuku..duuu......

ILA PIA KUNA WATU WANAIBIWA KWA DIZAINI HII MITANDAONI



You Might Also Like

0 comments: