Honey amka umwone bwege huyu kagonga gari yangu..........!! - alisema dereva wa Olpa.

17:06:00 Unknown 0 Comments

John ni mtumishi ktk idara fulani ya serikali jijini Dar, anaishi peke yake Tabata ktk nyumba ya serikali pia ana mchumba wake Venny ambaye anaishi kwa wazazi wake Kimara na kamfungulia Salon ya Wanawake karibu na kwao.

John anafahamika kwao Venny kwamba ndiye mume wake ajaye, na kutokana na umbali wa makazi yao, John alimnunulia Venny gari kwa ajili ya usafiri wa uhakika anapomuhitaji.

Siku moja John alipata safari ya kikazi kwenda Singida kwa muda wa siku kadhaa.

Baada ya kazi kwisha, John alianza kurudi Dar nyumbani akiwa na gari ya ofisini kwao na siku hiyo hakutaka kumwambia Honey wake kwamba anarudi kuhofia Venny angetaka kitu naye John amechoka.

Waliingia jijini mida ya alasiri na kukuta foleni Kali. Dereva wa John alijaribu kuovateki ili wawahi matokeo yake wakapata ajali kwa kugongana na gari ndogo aina ya Olpa.

Hapo ndipo kizaazaa kilianza kwa dereva wa Olpa Kutoa kashfa kwa John ambaye alitaka suluhu ya tatizo. 'we mjinga sana, mnagonga magari ya wanaume, hivi we gari kama hii unaweza kuinunua, Honey amka umwone bwege huyu kagonga gari yangu..........!! - alisema dereva wa Olpa.

John alipochungulia akagundua hiyo gari ndiyo ile alomnunua Venny namba T *** C**, na akamwona Venny ndani ya gari akiwa kalewa chakali wala hajitambui..

* Hivi kama we ndo John ungefanyaje? (wanaume)
* Kama ungekuwa Venny ungefanyaje? (wanawake)

You Might Also Like

0 comments: