Jamani nimechezewa mchezo mchafu
Mwezi wa kumi na moja mwaka jana nilifahamiana na binti mmoja ambaye ni rafiki na mpenzi wangu na wote walikuja kunitembelea.
Kudume nikashikwa kisawa sawa na uzuri wake na kujiapiza kuwa lazima nifanye yangu.
Si wajua tena sie madume tulivyo na uchu hata kama uwe na wife au mpenzi wa kuvutia kiasi gani lazima jicho likutoke na mate pia kwa kila unayepishana naye.
Nikafanikiwa kuipata namba yake na nikaanza kumrushia ndoano. Binti akaonyesha kutokubaliana na mawazo yangu na kila nikimweka sawa anajinasua na hataki kunipa nafasi na kutishia kumwambia mpenzi wangu.
Nikatilia kwa muda na hatimaye kuanza kutumia pesa na suprize za zawadi ili kumleta karibu jambo ambalo likaanza kuzaa matunda.
Tukaanza kutoka wote kwenda kusaka vinywaji mara chakula na nikaona dalili za kunipenda zinaonekana machoni kwake.
Mwezi wa kwanza nikawa nikimwomba nifanye nae mapenzi kidogo kwani ndio lengo kuu la mimi kuwa na uhusiano na yeye.
Baada ya vuta nikuvute hatimaye nikashinda vita na jumapili iliyopita tukakubaliana tukutane hoteli moja mitaa ya hapa mbeya ili alipe gharama zangu nilizotumia kwake.
Binti akanipigia mida ya saa moja na nusu usiku kuwa kafika na yuko chumbani nami nikamaliza bia zangu ingawa nilikuwa nishaanza kuona maluweluwe.
Kufika pake nikamwona amekaa akinisubiri na baada ya story natakakuanza mambo akaniomba azime taa kwanza na kumruhusu akazime kisha akaingia bafuni na kuja.
Alipofika bila maelezo nikaanza mambo na nilopomaliza nikainuka na kwenda bafuni kuwasha taa nikashangaa kumwona yupo bafuni na kabla sijafikiri nini nifanye nikarudi chumbani na kuwasha taa nikashtuka kumwona mpenzi wangu yupo kitandani.
Duh kumbe walinichezea mchezo
Hapa akili imeniruka sijui nifanyeje maana ni shidaaaaaa
0 comments: