Watu wabaya sana hebu ona huyu
Nilihitimu chuo kwa shida shida sana kama ujuavyo familia zetu za kimaskini na wakati huo hakukua na mkopo zaidi ya baba na mama kujikongoja.
Nikaamua kwenda Dar kutafuta ajira huku nikijishikiza kwa rafiki yangu ingawa mambo hayakwenda vizuri pamoja na kuandika barua kibao za kuomba kazi zisizo na dalili za mafanikio.
Nikarudi zangu kwetu huko kijijini na kuendelea kushirikiana na wazazi katika kazi za pale nyumbani na mida ya jioni nikawa pia najumuika na vijana wenzangu kubadilishana mawazo pale kijijini.
Nilikaa kijijini kwa muda na kuna siku moja jioni kuna kitu mzee mmoja nyumba ya jirani ambaye kwa pale kijijini alionekana kuwa na fedha alikiongea na kikaniudhi sana.
Eti, wewe john unakakaa hapa kijijini bila kuwa na kazi ya maana huoni kama unawaaibisha wazazi kwa kukusomesha na unakuja kukaa kaa hapa kama kijana wa mtaa??????
Nikamuuliza mzee unasema nawaaibisha kwa lipi?
Muda huo uchungu ukanijia nakuona kama baadhi ya watu hawajui magumu ya kutafuta ajira kama huna koneksheni nzuri.
Nikafilkiri nilivyohangaika na ninavyoendelea kuhangaika nipate kazi na kuwasaidia wazazi ambao wamenisaidia na kunipa moyo kuwa nitafanikiwa nizidi kutafuta kazi bila kukata tamaa.
Nikamwambia mzee, " baba kama umeongea kwa lengo la kunisaidia asante na kama lengo lako ni kunidharau basi namuomba Mungu nimwaminie na akuaibishe wewe"
Nikarudi na kuzidi kusali Mungu anipe uvumilivu na kunifungulia milango kwani yeye anajua mapito yangu.
Haikupita wiki siku moja jioni nikiwa narudi nyumbani kutoka mazoezini nilishuhudia mzee akiwa kalewa pombe na kavua nguo pale nyumbani kwake na watoto na mke wake wakijaribu kumficha kwa aibu.
Nikamsogelea na akaniona kisha akasema, " john watu wabaya sana ona naaibika"
Sikuongea kitu zaidi ya kuondoka nikisema Eeh Mungu asante kwa kudhihirisha unafiki wa watu mbele ya macho yetu.
Wiki chache baadae nikapata kazi na kwa habari za mtaani ni kuwa mzee yule hufanya miujiza ya kuziba riziki za watoto wa wenzie pale mtaani.
Kamwe usitetereke kwa maneno ya binadamu, Mungu hujua wakati muafaka wa kukupa mafanikio na kuwaaibisha wanafiki na wenye hila mbaya kwako.
Mungu ataendelea kutupa mafanikio katika mwaka huu kwa jinsi tutakavyo jikabidhi kwake na kujituma katika kazi zetu AMEN
Je ungependa kuwa mdhamini wa story zetu? Chat na admin whatsapp 0713317171
0 comments: