Jifunze hasara za kutangaza mipango yako sehemu isiyo sahihi

Mtafya alijikita katika biashara ya kahawa na baadae ikamtoa vilivyo na kuamua kuachana nayo na kisha kuingia biashara za vipuri vya gari.
Tabia yake ya ubabe na majivuno ikaanza kuwaudhi watu kabla ya kuamua kwenda kuwanunulia gari jipya aina ya RANGE ROVER ili aje kufunga midomo ya wapambe.
Akamwita jamaa yake aitwaye Nolesy wakutane katika bar moja maarufu na kisha wajadili suala la kwenda kulinunua gari hilo huko Dar.
Mtafya akamwambia Nolesy kuwa amekopa fedha kiasi na kesho yake ataliuza gari lake analolitumia kwa muda huo alilolinunua zaidi ya milioni mia ishirini mwaka mmoja uliopita na kuongeza fedha chache ili waweze kuinunua RANGE ROVER hiyo yenye thamani ya milioni mia mbili themanini.
Wakakubaliana kuwa fedha hizo zote mtafya atazichukua cash na kumpa Nolesy zikiwa kwenye briefcace ili asafiri mpaka dar siku ya tatu na kwenda Dar kwa usafiri wa basi na kisha kulichukua gari tayari kwa mkakati wa kuwaziba midomo wapambe nuksi.
Muda wote wakati wanaongea hawakujua kuwa kuna kaka jambazi alikuwa akifuatilia mazungumzo yao na kuwa naye tayari akaona kuna fursa ya kuwa milionea mtarajiwa, kagonga cheers na rafiki yake na kutokomea kwenda kujiandaa kwa safari kwani alishasikia na ni basi gani jamaa ataenda nalo dar kuifuata RANGE ROVER.
Siku ya tatu asubuhi saa kumi na mbili kamili gari likaanza safari na wote wakiwa safari moja yaani kaka jambazi na Nolesy.
Kaka jambazi akapanga wakifika sehemu yoyote kabla ya chimala asababishe umafia na kulichukua briefcase na asepe zake lakini kukawa na msululu wa magari mpaka wanafika makambako.
Mafinga mara iringa na baadae wakafika kula pale kitonga na kaka jambazi akaamua kuongea na dereva pamoja na kondakta wake ili asaidiwe.
Akawaambia kuwa, "Jamani shikeni 20,000/- kila mmoja wenu na naomba msaada kwa usumbufu utakaotokea, kwenye basi tuna ndugu yetu kichaa anatakiwa kupelekwa kwa mganga wa kienyeji pale ruaha mbuyuni, tulimpa dawa ya usingizi na sasa imepungua sasa tutakapo mshusha atapiga kelele maana ni msumbufu kweli"
Na wakati huo Nolesy alikuwa kalala baada ya kupiga viloba vilivyompa usingizi na kumfanya asahau hata kushuka kwenda kula jambo lililomfanya dereva na konda waamini na kumwonea huruma hasa kila aliposhtuka na kuzuga kwa kusoma gazeti kila alipokosa kontro ya usingizi na kumwangukia binti wa pembeni yake.
Nusu saa wakafika pale maeneo ya ruaha mbuyuni na konda akatangaza, "Samahani abiria kwa usumbufu hapa tutamshusha ndugu yetu ambaye ni kichaa na anakwenda kupata tiba za asili, poleni kwa ufumbufu utakao jitokeza......Asante"
Wakati huo yule rafiki kaka jambazi keshalishika briefcase na Nolesy ashachukuliwa na kaka jambazi halisia na anapiga kelele, "jamani hawa ni wezi siwafahamu nisaidieni ndugu wataniua......"
Abiria bila kujua nini chaendelea wao wakawasaidia wale majambazi huku wakimtakia mgonjwa apone haraka na baada ya vuta ni kuvute ya kumshusha Nolesy hatimaye basi likaendelea na safari.
Kaka jambazi wakamwamrisha Nolesy atembee kuelekea porini baada ya kuona wametembea umbali mrefu wakamwabia afungue briefcase na walipoona mzigo upo wakamuuliza sasa chagua......." Tukupe nauli urudi mbeya au unaenda dar?"
Jamaa akaamua kurudi mbeya, akiwa njiani kwa kuwa hata simu walimnyang'anya na hakuwasiliana na mtafya mpaka aliporudi nyumbani na baada ya kumwambia mtafya yaliyotokea amini usiamini mpaka leo ni mwaka wa tatu mtafya kazimia na ndoto ya RANGE ROVER kwishney.
Usitangaze biashara au mawazo yako sehemu isiyo sahihi
0 comments: