Hizi ndizo tabia za vijana wengi wa Kitanzania
Wazazi/walezi wako wamekusomesha hatimaye umehitimu shahada yako ya kwanza au hata masters au mafunzo mengine yoyote yale.Wamekutafutia kazi nzuri, salary scale yako imenenepa!
Kwasababu ndio kwanza unaanza maisha bado unaishi nao pale nyumbani. Zaidi sana wamekuazima na kale ka gari kao ambako walianzia maisha;ka-toyota STARLET ili ukabiliane na adha ya usafiri jijini.
Cha kushangaza hujawahi kupeleka nyumbani walau kilo ya sukari au kumzawadia baba angalau pair ya soksi au mama kitenge!
Wewe ni mtungi na anasa nyingine za dunia!
Amini amini nakwambia, wazazi/walezi wanaridhika na vitu vidogo sana, kupeleka kilo ya nyama nyumbani sio kuwalipa bali ni kuonyesha appreciation kwa fadhila walizokutendea.
Mioyo yao ikifurahi utabarikiwa na kufanikiwa zaidi........
0 comments: