Jinsi ya kukizuia kifo

22:45:00 Unknown 0 Comments

Miaka mingi iliyopita katika nchi moja ya mbali mwindaji mmoja alikwenda porini kuwinda kifo baada ya kusikia kuwa kifo kilikuwa kinamwinda yeye ili kimuue.

Mwindaji huyu alichukua begi ambalo ndani yake aliweka vitu vitatu ambavyo ni FURAHA, KICHEKO na TABASAMU.

Alipofika porini akakutana na kifo na kifo kwa haraka kikampiga yule mwindaji kwa kutumia MAUMIVU makali sana lakini yule mwindaji akachukua kwenye mfuko wake FURAHA na kuweza kuyatupa kule maumivu na Kifo kikaona kimeshindwa kumpa maumivu yule mwindaji kwani alijikinga kwa furaha.

Kifo kikampiga tena yule mwindaji kwa kutumia HUZUNI lakini wakati huu mwindaji akawa amechukua kwenye mfuko wake TABASAMU na kujikinga kiasi cha kifo kuogopa na kumshangaa huyu mwindaji kwa ujasiri wake.

Wakati huu kifo kikawa na hasira sana na kumkaba koo mwindaji ili kiweze kummaliza kabisa lakini bado mwindaji akawa amebakia na KICHEKO hivyo akacheka kwa sauti kubwa na kifo kwa mshtuko na mshangao kikakimbia na mwindaji akawa amefanikiwa kukishinda kifo na kurudi nyumbani.

Mfano huu unaendana na maisha yetu na jinsi tunavyoweza kukabiliana na mambo... 

Siku zote ukiweza kuishi maisha ya amani huku silaha zako kwa kila adui zikiwa ni kama za mwindaji huyu huku ukiongeza na UJASIRI hakuna linaloweza kukurudisha nyuma.

Na ili uweze kuishi na binadamu wengi ambao ni wanafiki wasiojali utu zaidi ya shida zao kwako na mwisho kukuacha na maumivu hata kama uliishi nao vyema kiasi gani basi huna budi kuwa na silaha hizi ili uzidi kusonga mbele.

Mungu atupe ujasiri wa kuyashinda majanga ya dunia hii pamoja na ongezeko la watu wasio na utu kwa watu wao.

AMEN

You Might Also Like

0 comments: