Kamwe sitosahau nilichomfanyia bibi harusi wangu mtarajiwa siku ya kumtolea mahari

22:13:00 Unknown 0 Comments




Haya mambo ya kuotaota ndoto yalishaanza kuniboa sana hivyo nikamsimulia rafiki na kupanga kunipeleka kwa mwanasaikolojia mmoja ili nipate ushauri.

Nikaenda mpaka ofisi ya kanselini na hatimaye nikaambiwa kuwa nilikuwa na msongo wa mawazo na hasira kali zenye elementi za kipalestina kuwa ningeweza hata kujilipua kama nisingewahi kupata kanselini.

Basi nikalala kama siku tatu za wiki iliyopita bila kuota ndoto na hata kama nilipitiwa na usingizi nikiwa kazini, bar, hotelini sikupatwa tena na ndoto zenye majanga kama ndoto zangu za awali.

Ijumaa nikapigiwa simu na rafiki yangu aitwaye morgan akaniambia anatarajia kwenda kutoa mahari siku ya ijumaa na kwa kuwa ni njombe hatakuwa na mizigo mingi wala mtu wa kumsindikiza hivyo twende wote kwani ndugu zake wao watatokea songea na tutakutana nao huko.

Kwa kuwa mahari ilitakiwa kutolewa saa  saba mchana basi mimi na morgani tukaanza safari saa moja ya asubuhi kuelekea njombe ndani ya gari tukiwa na viroba vya kupotezea mawazo na kumpa ujasiri bwana harusi mtarajiwa.

Tukikuvya vile viroba na tulivyofika chimala tukawa tumeishiwa na kuamua kusimama kwa muda kununua pombe nyingine.

Dakika chache tukawa barabarani tukiwa na pombe zetu na safari ikaendelea huku tukowasiniana na shemeji ambaye ndio anaenda kutolewa mahari akituhakikishia kuwa tumewahi sana.

 Kituo cha pili ikawa makambako na muda huo ikawa saa nne ya asubuhi. Tukapokelewa na marafiki na kupata supu pale na kazi ya pombe ikaendelea huku tukipewa mbinu za kutolea mahari na kuwa majasiri kujibu maswali ya mitego kutoka kwa wakwe.

Muda huo pia nilikuwa nasoma ukurasa wa tabasamu na fuledi nikaanza kuona nao hausomeki ikanibidi nitoke haraka nje na kwenda kuomba limao na maji ya kunawa usoni kupunguza pombe kichwani.

Wakati huo na morgan akawa amenitumia ujumbe kupitia whatsapp kuwa nae anahisi alkoholi inapanda, tukaondoka na kuanza safari ya kwenda njombe tukiwa na pombe nyingine tulizofungiwa na marafiki za kunywa njiani.

Kazi iliendea huku tukifurahia mziki wa gari letu mapaka nusu saa baadae tukawa njombe wakati huo ilikuwa ni saa saba na madakika shemeji yaani mke mtarajiwa wa morgan akatuomba tukae sehemu atatuita na baadhi ya dugu wao wakawa pia wako njiani.

Tukaanza tena shughuli yetu ya bia na wakati huu tukijipa imani kuwa masuala ya mahari hayana uzoefu wala ujasiri jambo la msingi ni kuweka vitu kichwani yaani pombe kukaa sawa sawa.

Bila mimi kuamka pale na kwenda kwenye gari kuchukua simu na kushuhidia sms na misses calls kibao kwenye simu zetu tulizozisahau garini basi saa tisa ingetukuta pale.

Tukainuka haraka na kuelekea kwenye mahari baada ya kuwapitia ndugu zetu ambao walishaanza kuchukizwa na kuchelewa kwetu.

Wakaingia baadhi ya ndugu pale kwa wakwe na kuniacha mimi na morgan tukiwa garini. Morgan akafungua mfuko na kunirushia viroba viwili na naye kufungua vyake na kusema hata kama tumechanganya mapombe ila sio mbaya kupiga hivi kujaziajasiri ili tusiumbuke.

Tukazinywa sana na ikafika muda wa morgan kwenda kutambulishwa hivyo tukanyanyuka na kuelekea ndani.

Wakati huo nikawa naona dunia inazunguka na morgan akaniambia miguu anahisi haina nguvu.

Nikamwambia ajikaze na tukafika pale ndani akiwa nyuma yangu mara mziki ukawashwa na shamra shamra ukafika muda wa kusimama ili morgan asalimie ndugu..... 

Aliposimama akakosa balansi na kwenda moja kwa moja mpaka meza ya wakwe na kutaapikia nikasimama kwa haraka nimsaidie huku shemeji akija kumwokoa basi mie ndio nikamtaapikia shemeji yangu kabla ya kushtushwa na kibao kutoka kwa mhudumu wa bar kumbe mikonyagi imenizidi hapa bar na nililalal ile wananiamsha nimefanya yangu..... 

Hizi pombe hizi duuuuh hebu soma maoni ya wadau HAPA

You Might Also Like

0 comments: