KWA NINI NAWAPENDA WANAWAKE.....
(Soma hii mpaka mwisho)
Mme na mke walikuwa wamekaa wanatazama TV mara mke akasema, “Ushakuwa usiku sasa, nimechoka ngoja nikalale”
Akanyanyuka na kwenda jikoni akawaandaa samaki wa chakula cha siku ya pili mchana, akapika chapatti kwa ajili ya chai ya siku ya pili asubuhi kisha akachemsha chai kwa ajili ya watoto asubuhi.
Akaiandaa meza na kuweka kila kitu muhimu kama vile vijiko, vikombe, sahani, cocoa, majani ya chai nk kwa ajili ya chai ya asubuhi.
Kisha akaingia ndani na kuandaa nguo za kuvaa mmewe asubuhi na watoto wake waendao shuleni, akaja sebuleni na kuondoa makaratasi na kuweka vitu sawa baada ya watoto kuvichezea, Akachukua simu na kuzichaji akaweka kila kitu sehemu yake.
Akajinyoosha ili aende kitandani lakini aka kaka mezani na kuandika karatasi ya kumkumbusha kwenda shuleni, akachukua kadi na kuandika kwa ajili ya kuwatakia birthday marafiki zake siku ya pili na kuziweka kwenye bahasha.
Akaorodhesha mahitaji ya kuchukua sokoni siku ya pili yake akitoka kazini na kuweka vitu vyote karibu na mkoba wake. Akaingia bafuni akauosha uso wake na kujikausha, akapiga mswaki ….. Mme akamwita, “Nilifikiri umeenda kulala kumbe bado.” “Ndio nataka kulala sasa,” akajibu.
Akanyanyuka na kwenda kuhakikisha milango yote imefungwa na kuifunga. Akapita chumba cha watoto na kuweka neti vizuri na kuongea na mmoja aliyekuwa akimalizia kazi za shule.
Akawategea kengele ya saa ya kuwaamsha asubuhi wasichelewe kujianda na kuhakikisha taa zimezimwa na radio pia akarudi chumbani kwake na kuweka nguo zake vyema za kuvaa kesho yake. Kisha akasali na kumshukuru Mungu kwa kumaliza majukumu ya siku salama.
Mme yeye alisimama pale alipokuwa amekaa akitazama TV, akaizima TV na kujisemesha, “Naenda kulala sasa" bila kujua anamwambia nani muda ule.” Na akaenda kulala bila kufanya chochote wala kuwa na wazo la kufanya chochote
Umeona umuhimu wa mwanamke hapa? Share ujumbe huu kwa kuonyesha umuhimu wa wanawake …
Wao ni chimbuko la furaha zetu na mafanikio yetu…
Share pia ujumbe huu kwa kila mwanamme lia nao waone umuhimu wa mwanamke katika Maisha yao……!!!
Amen
0 comments: