Ni rahisi kufikiri unawaharibia watu kumbe unajiharibia
Mzee mmoja alianza hofia kuwa yawezekana mkewe kaanza matatizo ya kutosikia vizuri.Hivyo ikambidi amtafute daktari wa familia na kumsimulia mkasa mzima.Baada ya daktari kumsikiliza yule mme vizuri, akamwambia kuwa sasa atahitaji akirudi nyumbani amfanyie jaribio moja mkewe ili majibu yake yaweze kumpa dokta mwanga wa kumsaidia kulitambua tatatizo na yule mama apone.
Daktari akamwambia, “ ukirudi nyumbani simama futi 40 kutoka kwa mkeo na kwa sauti ya mazungumzo ya kawaida ongea neno ili uone kama atasikia na kama hatasikia simama karibu futi 30 ukimsogela , kama hatishoshi ongeza zaidi futi 20 mpaka atakapo kusikia”
Jioni yake mzee akiwa sebuleni na mama akiwa jikoni anaandaa chakula cha jioni, baba akiwa sebuleni akamwita mkewe na kuuliza, “Mpenzi tuna kula nini leo jioni?” lakini mke hakujibu.
Mzee akazidi kusogea futi 30 karibu akamuuliza tena, “Mpenzi tuna kula nini leo jioni?” lakini pia mke hakujibu, mzee akasogea tena futi 20 karibu na jikoni na kumuuliza tena, “Mpenzi tuna kula nini leo jioni?” mara hii mke hakujibu tena.
Basi ikambidi yule mzee amsogelee mpaka karibu yake na kumkumbatia mgongoni huku akimuuliza tena “Mpenzi tuna kula nini leo jioni?” mkewe akamjibu,” mme wangu nimepika kuku” mbona nimekujibu tangu uko sebuleni ina maana hukunisikia?
Mzee yeye alidhani mkewe ndio mwenye tatizo la kutomsikia mtu akiwa mbali yake kumbe yeye mzee ndio mwenye tatizo la kutosikia mtu akiwa mbali.
Ndio ilivyo katika Maisha yetu ya kila siku, tunaweza tukafikiri kuwa wenzetu ndio wenye matatizo zaidi lakini kumbe sisi ndio wenye matatizo zaidi.
Pia ni vyema kutokuwa wepesi wa kuhukumu au kueneza jambo lolote tunaloliona kuwa ni baya bila ya kuangalia sisi tupo upande gani katika uvumi huo.
Ni rahisi kufikiri unawaharibia watu kumbe unajiharibia
0 comments: