Nilipomakliza sala hii nilijikaza na kujikamua kwa nguvu nikishindana na maumivu ya kamba ambayo ilianza kunitoa uhai kwa kuikaba shingo yangu

06:58:00 Unknown 0 Comments


Sikuwa nakaa nyumba moja na mpenzi wangu Salome kwani yeye alikaa mtaa wa nne kutoka pale nilipokuwa nakaa.

Mara nyingi alikuwa akinitembelea na kunisaidia baadhi ya kazi pale nyumbani hasa hasa masuala ya usafi na kuandaa chakula cha pamoja.

Salome aliumbika sana na kama haitoshi kumpata kwake ilikuwa ni vita nzito kati ya kabwela mimi, wenye fedha zao na kila kijana aliyeanza kuota ndevu kidevuni mwake  huku sauti ikianza kutoa muugurumo pale mtaani.

Nilipewa majina mengi ya ushindi kwa kumiliki totoz la kidigo tena toto ambalo kila mtu alitamani kulimiliki na kuishia kula kwa macho huku kijana nikijimilikisha kiulaiiiiini.

Nilikula nae good time kila sehemu nikiwa nae na kweli kazi nilowaonesha pale mtaani yaani lengo kubwa ni kuifunga midomo ya mapuuzi wote wenye kutaka kumiliki hata visivyo vya uwezo wao.

Kuna ugonjwa mmoja ukaanza kuniathiri tena sio kidogo na ugonjwa huo ni ule wa wivu, sikutaka hata sekunde salome aongee na mtu mwingine iwe kwa simu, facebok, whatsapp au live kwani nilivimba na kufura kwa hasira.

Ijumaa moja niliwahi kutoka kazini na kuamua kurudi nyumbani ili nijipumzishe kidogo. Nilipoingia mlango ulikuwa wazi na nilipochungulia chumbani akikuwa kajilaza pale kitandani.
Sikutaka kuingia ili nimpe muda apumzike kwani alikuwa kafanya usafi wa nguvu mle ndani. Nikiwa pale simu yake ikaingia sms kupitia whatsapp na ikaonesha ilitoka kwa mwanaume akimsifia jana yake kwa penzi zito.

Hasira ilinipanda na kuanza kuamini ya kuwa salome hakuwa wangu tu ila alikuwa na kundi kubwa la wapenzi...

Nikaamka kwa hasira na kumpiga ngumi ya kichwa na hakuamka tena zaidi ya kurusha rusha miguu na hatimaye nikagundua kafia pale kitandani maana mwili ulipoa na kuwa wa baridiii.

Niduwaa kwa dakika na kuona mwili ukiishiwa nguvu na kama haitoshi ujasiri ukanipotea nikakimbilia sebuleni na kukaa pale kwa dakika kadhaa nikijiuliza ni nini cha kufanya.
Macho yangu yakakutana na chupa kubwa ya  Grants iliyokuwa kabatini nikaichukua na kianza kuinywa nikiamini kuwa salome atazinduka.

Yalipita masaa kadhaa kukiwa hakuna dalili ya salome kuamka na wakati huo ilikuwa imetimia saa saba usiku.

Wazo likanijia kuwa akikaa pale ndani itakuwa kesi hivyo nikambeba na kupita naye baadhi ya vichochoro na hatimaye kuingia pori moja na baada ya mwendo ulionichukua dakika kadhaa nikajikuta nipo katikati ya pori hilo na kumtupa pale salome na haraka nikarejea nyumbani.

Nilirudi na kulala nikiwa nimechoka sana baada ya kuubeba ule mwili mzito na pale kitandani nikaona simu ya salome ba baada ya kuikagua na kurudi sebuleni kuiangalia ile ya sebuleni nikagundua ile haikuwa yake ila ni ya rafiki yake kwani kuna ujumbe ulimtaka ampelekee simu yake mapema.

Nikaanza kutokwa na machozi nikiona kabisa kuwa nimeenda nje ya mstari na kusababisha mauaji yasiyo na hatia na kama haitoshi nikaanza kujutia kila hatia kwani muda huu na hasira zilishaiishia.

Nilala kwa muda kabla ya kushtushwa na simu ya rafiki yangu akinipa taarifa za kupotea kwa salome nikajifanya kushangaa na baada ya mazungumzo kucheki muda ilikuwa ni saa tisa ya mchana ya siku ya pili.

Nikajivuta mpaka bar moja na kupata mchemsho ingawa kila mtu alikuwa akiniambia siko kama kawaida yangu na baadhi wakinipa pole ya kupotea kwa salome wengi wakidaia atakuwa kanikimbia kijanja kwenda kwa wenye hela zao.

Nilirudi nyumbani kama saa nne usiku na kulala, lakini mida ya saa saba usiku akanitokea kwenye ndoto salome na kusema watu wameanza kunitafuta hivyo pale uliponificha watagundua na utafahamika kanihamishe.

Nikaamka na kwenda mpaka pale na kumwamisha mpaka kichaka kingine na kumweka nikiamini yuko salama na kurudi zangu nyumbani.

Siku ya pili watu wakawa wameanza kukusanyika kwa mjumbe ili kuanza kumtafuta salome nami nikiwepo.

Tulimtafuta siku nzima bila mafanikio na baadae tukapumzika baada ya kutokumwona  na usiku kama kawaida salome alinitokea na kunipa tahadhari kuwa angeweza kuoonekana hivyo nikamwanisha tena.

Niliendelea na kumwamisha kila mara huku nikiumia na kuona kama ni suala la upuuzi sana. Na nakumbuka ilifika mahali nikawa sina amani kabisa.

Nilikuwa nikilia kwa uchungu nikiulaani upuuzi wangu wa kumpiga salome kwa wivu wa kipuuzi na huku akiwa hakufanya kitu huku nikeenda kumwamisha kule nilikomficha na muda huu alikuwa kashaanza kutoa harufu mbaya.

Kazi ile iliendelea kwa siku mbili mbele kabala ya kuja kushikwa na polisi wa doria usiku mmoja nikimwamisha kwenda kumficha mahali pengine huku akiwa kashaoza.

Kila mtu siku ya pili yake alishangaaa na hatimaye nikapelekwa mahakamani na kesi ikaanza kuungruma kwa muda wa miezi kadhaa.

Niliumia kwa maamuzi yangu ya kijinga na kuona adhabu yoyote ile ilikuwa stahili yangu na kuamini kuwa nilitakiwa kuwa matunda ya wivu wangu wa kijinga.

Hakimu aliongea mbele ya umati ule kuwa baada ya upelelezi kukamilika na kuridhishwa na pande zote yaani utetezi na mashata kuwa nitahukumiwa kunyongwa.

Wakati huu sikulia kwani hata machozi yasingetoka kwa jinsi nilivyolia kwa muda mrefu na kujijutia upuuzi wangu... Nilatabasamu na kimwomba kimoyomoyo salome anisamehe kokote aliko.

Siku chache baadae nikawa nipo sehemu ya kunyongewa na mchungaji akawa yuko pale akishuhudia kunyongwa kwangu.

Nikaomba aniniongoze sala ya BABA YETU kama ifuatavyo:

Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani kama huko mbinguni.
Utupe leo riziki yetu.
Utusamehe makosa yetu,
kama sisi tunavyowasamehe waliotukosea.
Na usitutie majaribuni,
lakini utuokoe na yule mwovu.
Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na
utukufu, hata milele .
Amen.

Nilipomakliza sala hii nilijikaza na kujikamua kwa nguvu nikishindana na maumivu ya kamba ambayo ilianza kunitoa uhai kwa kuikaba shingo yangu taratibu nikaanza kuhisi uhai ukinitoweka huku harufu mbaya ya kinyesi ikitawala na kilio kwa mbali kabla ya kuchapwa ngumi na mama mwenye nyumba kumbe muda huo wote nilikuwa naachia kimba kitandani huku nikimalizia ndoto yangu.....

Hizi ndoto bwana tatizo

You Might Also Like

0 comments: