KWANINI BIASHARA YA BLOGGING HAILIPI INALIPA
Sikia hii kali kutoka kwa Bwana Mushi
mwanzilishi wa NIPENI DILI MASELA ambaye
alipata kusikia mazungumzo kati ya mzazi na
kijana wake ambapo mazungumzo yalikuwa hivi:
Mzazi: Ukimaliza lasaba una mpango gani?
Mtoto: "Nimepanga kuanzisha blogu"
Kichekesho hapo juu kinatukumbusha namna
ambavyo suala la blogging limeonekana kama
aina fulani ya biashara ambayo wengi wetu
tungependa kuifanya. Na hata wengine kuamini
kuwa wanaweza kujiajiri kupitia biashara ya
blogging.
Nimekuwa kwenye fani hii ya blogging kwa
mwaka wa tatu sasa, na pia nimekuwa
nikijifunza kupitia kwa bloggers mbalimbali, na
kusoma makala za kitaalamu kuhusu fani hii
inayokuwa kwa kasi sio tuu Tanzania, bali
duniani kwa ujumla. Yafuatayo ni mambo ya
msingi unayoweza kuchunguza ili kujua kama
blogging itakuwa na faida kwako au la:-
1. Gharama za kumiliki na kuendesha blog
Ingawa ni kweli kuwa ni bure kabisa kuandikisha
na kuifanya blog yako irushwe hewani iwe kwa
wordpress.com au blogger.com, kumbuka kuna
gharama nyingine nyingi kama kweli unataka
blogu yako iwe na ubora wa ushindani katika
soko. Gharama hizo ni:-
Gharama za fedha : Inapendeza pale
unapokuwa na anuani maalum ya blog yako
yaani badala ya kuwa na
www.blogyako.blogspot.com, unakuwa na
www.blogyako.com . Kupata anuani maalum
(domain) itakubidi utumie fedha.Pia badala ya
ku host na blogger au wordpress unaweza amua
kuhamishia blog yako kwa taasisi zenye ku host
kwa malipo. Gharama nyingi ni malipo ya
kutengeza vizuri muonekano wa blog yako,
gharama za usafiri kufuatilia habari, gharama za
kuwepo mtandaoni – internet bundles, gharama
za simu na pengine chakula unapokuwa
unahangaikia kupata taarifa za kuweka kwa
blogu yako.
Gharama zisizo za fedha: Kuna gharama
nyingine kama vile muda unaopoteza
kushughulikia makala za blogu yako na kutafuta
wasomaji. Pia gharama za usumbufu wa kiakili
pale unapojikuta ukikata tamaa kwakuwa blogu
yako haiendi vizuri, au unapopata upinzani usio
wa maana toka kwa watu mbalimbali, hususani
bloggers wenzako.
2. Mapato yatokanayo na blogu
Mapato ya moja kwa moja: Chanzo kikuu cha
mapato kwa blogu ni matangazo. Unaweza
kuwalipisha watu binafsi, makampuni, serikali
na hata asasi mbalimbali zinazotaka kuweka
matangazo kwa blogu yako. Chanzo kingine cha
mapato ya matangazo ni kupitia huduma ya
Google Adsense , ambapo blogu yako ikikidhi
masharti ya Google Adsense , basi utaanza
kuona matangazo yakiwekwa kwenye blogu
yako, baada ya wewe kuwa ume omba huduma
hiyo iwekwe kwa blogu yako. Google itakulipa
commission kwa matangazo wanayoweka.
Mapato mengineyo: Kuna nyakati blogu
inaweza kukuingizia mapato kupitia ubunifu
wako wa kuitumia kujenga mapato sehemu
nyingine. Mfano blogu yako inaweza kukufanya
ukajenga mtandao mkubwa wa ‘watu muhimu’.
Hii itakurahisishia dili nyingine utakazotaka
kufanya hapo baadae. Hata hivyo kujenga
mtandao imara ni kazi kubwa. Soma hapa JINSI
YA KUJENGA MTANDAO WENYE MANUFAA. Ukiwa
na bidii katika blogu yako utalazimika kujifunza
mambo mengi mapya,ya kiteknolojia, uandishi
makini, marketing na hata namna ya kujenga
mahusiano bora na watu wengine. Hizi ni faida
kubwa sana kwa maisha yako.
3. Vifaa vya kazi: Ili kufanya kazi zako za
blogging kwa ufanisi unahitaji kuwa na
kompyuta, hususani laptop ili uwe na uhuru wa
kufanya kazi mahali popote. Kumbuka pia
unaweza kutumia smartphones kuandaa na
kurusha hewani makala zako. Unahitaji kuwa na
modem au sehemu yoyote ya uhakika ya kupata
huduma ya internet.
4. Kazi za blogger
Kuandaa makala
Kutafuta habari
Kupiga picha
Kupost
Kutafuta wasomaji
Kutafuta wanunuaji wa nafasi za matangazo
Kuendelea kujifunza mabadiliko mapya
Kuweka Malengo na kusimamia ukuaji wa blog
0 comments: