Maalumu kwa wale wanaopenda kulalamika katika kila hali au hatua za maisha yao

09:48:00 Unknown 0 Comments

Ikitokea siku ukaamka na kugundua mguu au miguu yako yote miwili inauma, basi wewe anza kujifunza kutembea na mguu au miguu inayouma ukitafakari njia za kwenda kujitibu au kupata matibabu.

Kukaa kitandani na kulia ukitegemea kuna malaika atakuja kukunyanyua kitandani na kukupa tiba sahau...... kwani utaishia kufa kwa njaa pia.

Hivyo hivyo ukijikuta uko kwenye matatizo ya maisha anza kujifunza kutumia mianya midogo inayojitokeza kwako huku ukiangalia namna ya kujitatu katika tatizo hilo.

Kundelea kupiga kelele na kulalamika hutafanya chochote zaidi ya kutukaribisha wana habari kuandika kila habari yako ambayo kama ukibahatika kuipata/soma unaweza kufa kwa presha.

Maisha sio kulalamika au kusubiri watu wakupe miujiza...... KOMAA mwenyewe hata kaburini utaingia peke yako

You Might Also Like

0 comments: