Makubwa!!!!!!!!!!!!! Akaunti feki ya facebook yampa tumbo joto kijana mwingine
Kama kawaida yangu nilikiwa safarini naenda zangu mkoani kikazi na nikiwa sina cha kufanya ndani ya basi watu wamelala basi nikaamua kuichukua simu yangu na kuanza kuperuzi mtandaoni.
Nikakutatana na friend request ya binti moja na kwa kuwa nimeshakuwa na majanga sana hapa fb nikaona kabla ya ku-accept basi nimcheki kwanza kama ni besti na marafiki zangu wote.
Baaa ya kukuta ni rafiki na baadhi ya marafiki zangu nikamkubalia na tukaanza kuchati na bibie akawa akinipa text za adabu na safari ikawa fupi sana.
kwa maelezo yake ni kuwa yeye anakaa pia tabata kimanga kwa hiyo tukakubaliana siku ya pili jioni nikiwa narudi basi tukutane ili aweze toa upako kidogo.
Na siwajua tena mabinti walio wengi hapa fb maharage ya mbeya... maji mara moja tuu, yaani akiona tu kwenye profile una kagari bila hata ya kujua wewe ni mfanyakazi wa car wash yeye anajua una hela sana... usiombe upige picha sehemu ya kaunta ndefu yaani lazima umpate maana atajua wasaa wa good time ndio huo..
Siku ya pili nilimaliza kazi mapema mkoani na kuwahi kufika dar mida kama ya saa kumi na moja vile, kwa kuwa njiani tulikuwa tunaendelea kuchati na bibie nilisha m-mpesa akawa tayari kashaingia hoteli moja na yupo kwa room ananisubiri mzee wa shoka au papaa nije sababisha mambo.
Nikafika mpaka chumbani nikaoga zangu na kisha nikamtoa mtoto twende tukapate bia moja mbili na chakula na baada ya hapo tukarui room tena.
Ebwana yule binti amini usiamini ni mzuri na ngozi ya asili na hana mdhamini wa mwili wake kama mchina au karoraiti bali ni asili tupu imemzunguka, sitaki kukuambia zaii ila wewe jua ni mzuri.
Tukiwa tupo pale ndio nakaribia itikadi zangu mara mlango ukangongwa na mhudumu, ile nashangaa wakaingia majibaba kama wanne na hawakuongea lolote wakanisachi na kuchukua kila kitu mpaka nguo zangu na kuniacha mtupu kisha wakamchukua binti wao na kuondoka.
Yule mhudumu tena wa kike akawa akinikodolea mimacho nikamwomba kama angeweza kunisitiri, akenda mapokezi na kuchukua tracksuit zake na kuniletea pale..nikaona sasa ilishakuwa taabu nikakimbia na kudaka boda boda na kuwahi home.
Nikafika home mida ikiwa bado kama saa tatu vile naingia ndani mke ananiuliza, "baba naninii ulipitia wapi? Maana nimefika hapa na kuona mabegi yako nje nikayaingiza ndani"...
Nikaona hajagundua kitu na kwa kuwa kazoea kuniona navaa nguo za mazoezi nafikiri akajua nimenunua huko mkoani na ikawa inaonyesha nyumbani hapakuwa na mtu.
Ikabidi nimjibu fasta nimwambie nilifika nikampa mtu ayalete mara moja mie nikawa napata bia na marafiki.
Na wakati nikiwa bado sielewi kinachoendelea ikaingia sms kutoka kwa binti niliye wahi kumtelekeza na mtoto anasema, " wewe si unajifanya mjanja sasa nakupa siku chache uanze kuleta matumizi au utaona moto wake ya leo ilikuwa trailer"
Hapa nimechanganyikiwa kabisa na sijui niripoti polisi au nifanye nini hawajanidhuru wala kuchukua chochote bali wamevileta nyumbani................... Nimedata
Sijui nini kitafuatia na kumwambia wife itakuwa patashika

0 comments: