Meseji kutoka kwa mchepuko feki imeokoa ndoa yangu sasa mme ananitunza

14:25:00 Unknown 0 Comments


Mme wangu alifikia hatua ya ajabu sana kiasi kwamba kila siku ilikuwa ni zaidi ya ugomvi na hakuna tena furaha tuliyokuwa nayo mwanzo pale nyumbani.

Alinilaumu na kunipiga kila akiona nina ongea na mwanaume na mbaya zaidi hata akiwa ni mfanyakazi mwenzangu.

Kila sms iliyoingia kwenye simu yangu ikagundulika kuwa ni ya mwanaume basi lazima nipate mong;oto hata kama ni marafiki na wafanyakazi wenzangu tuliozoeana na tusio na mahusiano mengine.

Nilianza kukonda na kuona sasa ndoa ni karaha na mbaya kuliko vyote hata ofisini na marafiki wakaanza kuona napungua na sina furaha muda wote.

Kiukweli mme wangu alizidisha wivu ambao sijui ni wa nini na kilichoniumiza kuna siku niliwahi kurudi nyumbani na boss wangu akawa amenitumia sms akisema anaomba tuonane ofisni na wengine kuna emergency.

Mme alichukua ile sms na kumpigia na kumtukana sana na kisha kunipiga mimi bila kujua ilikuwa na sms ya kiofisi na kitengo nilichokuwa nikisimamia kilitakiwa kuandaa baadhi ya vitu kwa ajili ya kwenda field.

Niliondoka nikiwa nimevimba na kwenda ofisni ingawa nilihisi boss amechukia nikamwomba msama na namshukuru Mungu alikuwa mwelewa.

Baada ya kazi rafiki yangu mmoja wa kiume pale kazini akaniita na kuniambia anahisi sina amani katika ndoa yangu na kwa kuwa ni rafiki nimshirikishe nami nikaona sina jinsi ngoja iwe hivyo.

Baada ya kumsimulia akaniambia sasa kama nataka kuiokoa ndoa yangu kutoka kwa wivu wa mme wangu basi niwe na roho ngumu naye kuna assignment atanipa tuifanye kwa pamoja nikakubali.

Akaniambia sasa nisiogope hata kama atanipiga siku mbili ila ataipata adamu yake tuu mimi nikirudi jioni niwe naweka simu yangu on yeye atakuwa akituma meseji zake na mimi nikiulizwa niseme simjui atumaye hata nikipigwa.

Jioni ya pili nikiwa nyumba meseji kutoka namba ngeni ikaja na simu alikuwa nayo mme wangu namni nikiwa jikoni naandaa chakula cha usiku.


Mme alikuja sipi jikoni akiwa kafura na kunionyesha  meseji iliyoandikwa, " Mama Alvin, vipi mbona jana hukupitia tena nyumbani au huyo kunguru asiyethamini uzuri wako kakupiga tena? Nijibu mpenzi"

Mimi nikasema simhafamu kweli akanipiga nami nikaacha kupika na kwenda chumbani kulia ili watoto wasione kinachoendelea na huku nyuma wakaendelea kuchati naye.

Siku ya pili kazini rafiki akasema tulia tu sasa jamaa atakuwa anaumia, jioni yake ikaja sms nyingine ikisema, "mama alvin mimi naenda safari iringa ila kama zile hela laki 400,000 nilizokupa juzi za shoping zimeisha nitakutumia fedha ya kuwanunulia watoto wa huyo mbwiga nguo za sikukuu"

Safari hii hakunipiga akaondoka na kwenda bar, ana liporudi alikuwa kalewa sana asubuhi alipoamka akaichukua simu na kuona kuna sms imeandkiwa " Mama alivin jamaa yako jana alinitafuta sana sikupokea simu angalia asije akaziona hela akaanza kuzitumia mimi nimekuwekea bank"

Mme aliamka na kwenda bank na hakuona chochote ila aliporudi kwa mara ya kwanza nikashangaa kuona karudi na nguo za watoto na baadhi ya zawadi zangu na wiki ile sms haikuja tena.

Wiki moja baadae ikaja sms ikisema, " mama alvin siku hizi umenichunia au jamaa haklupigi tena uje nikuliwaze maana huyo kunguru hafai kupewa mwanamke wa kuishi nae"

Nikaona mme wangu akizidisha mpanzi na mpaka leo ni mwaka wa nne hajawahi kushika simu yangu na sijawahi kupigwa na mapenzi kazidisha zaidi na zadi. 

Kila siku ninamshukuru yule rafiki kwa kuutunga mchezo wa sms feki zilizookoa ndoa yangu na nilipomsimulia mme wangu alicheka sana sana na kusema ila zimenifundisha kukuamini na kukupenda 



Kama umenielewa comment "Mwanamke hapigwi" kisha share sana wengi wapate

You Might Also Like

0 comments: